YANGA KISICHO RIZKI HAKILIKI …yabanwa nyumbani na Ndanda FC
Ikicheza
nyumbani, Yanga ya Dar es Salaam imelazimishwa sare ya bila kufungana
na Ndanda FC ya Mtwara katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Uwanja wa
Taifa.
Yanga ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini washambuliaji wake walikosa umakini wa kuchomeka mipira wa wavuni.
Nafasi
ya wazi zaidi kupotezwa na Yanga ilikuja dakika ya 77 wakati Amis
Tambwe alipomimina krosi ya chinichini kutoka upande wa kulia na mpira
ukamkuta Danny Mrwanda akiwa yeye na wavu lakini kwa mshangao wa wengi
akapaisha mpira juu.
No comments:
Post a Comment