THIERRY HENRY ASEMA CHELSEA ITATWAA UBINGWA ENGLAND … amvulia kofia Jose Mourinho
Mshambuliaji
wa zamani wa Arsenal na Barcelona Thierry Henry amesema anaamini
Chelsea itatwaa ubingwa wa Premier League kwa sababu Jose Mourinho
anajua namna ya kupata matokeo mazuri hata pale timu yake inapocheza
vibaya.
Thierry
Henry aliyekuwa mchambuzi wa mechi ya Chelsea dhidi ya mabingwa
watetezi Manchester City katika dimba la Stamford Bridge, anasema
Mourinho anatakiwa ajihesabu kuwa ni mwenye bahati kwa kuepuka kipigo na
kuambulia pointi moja.
Katika
mchezo huo uliomalizika kwa sare ya 1-1, City ilicheza vizuri zaidi na
kutengeneza nafasi nyingi za magoli ingawa umaliziaji ulikuwa tatizo.
Chelsea
ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Loic Remy lakini wakawa chini
ya shinikizo kubwa baada ya David Silva kusawazisha na kufuatia hali
hiyo Thierry anasema klabu hiyo ya London imeonyesha alama zote za kuwa
mabingwa wapya wa Premier League.
“Tunastahili
kuwapa pongezi Manchester City kwa kuchukua pointi moja ‘darajani’?
Hapana,” alisema Henry kupitia Sky Sports baada ya mchezo huo.
“Walisawazisha, wakamiliki sana mpira pamoja na kuwa na nafasi nyingi zaidi za kufunga. Hawakushinda.
“Hivyo ndivyo
wanavofanya Chelsea. Wakati fulani wanaweza wasicheze vizuri lakini
wakashinda 1-0. Wamehangaika sana leo (jana) lakini hawakupoteza mchezo.
Hii ndio sababu inayonifanya niamini kuwa Chelsea itatwaa ubingwa.”
No comments:
Post a Comment