Waziri Mkuu Mizengo Pinda atoa rai kwa wakulima na wafugaji wote nchini kujikubali ni Watanzania
Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maenedeleo ya Makazi na Mbunge wa Mbunge wa Manyoni Mashariki, Kapteni Mstaafu John Chiligati, akichangia hoja.
Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo, akichangioa taarifa ya kamati teule.
Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Sabrina Sungura aichangia hoja.
Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman akichangia taarifa.
Wabunge wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya mkutano wa Bunge kuvunjwa.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Charles Mwijage, akisalimiana na Mke wa
Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda(kulia) baada ya Bunge kuvunjwa.Katikati ni
Mbunge wa Viti maalum (CCM) mkoa wa Singida Diana Mkumbo Chilolo.
Baadhi ya wafugaji waliohudhuria Bungeni wakizaungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) baada ya kuvunjwa kwa Bunge.
……………………………………………………………………
Na Lorietha Laurence-Maelezo,Dodoma
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ametoa rai kwa wakulima na wafugaji
nchini kujikubali kuwa wote ni Watanzania na wanahaki ya kuishi popote
bila kuvunja sheria.
Amesema hayo Bungeni Dodoma alipokuwa akipokea na kukubali
taarifa na mapendekezo iliyotolewa na kamati teule ya Bunge ya
kuchunguza na kuchambua sera mbalimbali zinazohusu masuala ya
Ardhi,kilimo,mifugo,maji na uwekezaji.
“Nimepokea mapendekezo yote yaliyotolewa na kamati na ninaahidi yatafanyiwa kazi kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania” alisema Pinda Aliongeza kuwa kwa utekelezaji wa awali serikali itauunda tume maalum ya wataalum mchanganyiko na tume ya makatibu wakuu ili kuweza kupitia taarifa hizo na baadaye kuwasilisha kwa ajili ya utekelezaji.
Aidha alisema ni wajibu wa Wizara ya Ardhi kupima ardhi katika maeneo mbalimbali na kwa wale wanaokiuka taratibu wachukuliwe hatua madhubuti ya kuwawajibisha. Hata hivyo Waziri Pinda alisema kuwa kuna umuhimu wa kutolewa kwa elimu ya kuwahamasisha wananchi umuhimu wa kulinda na kuitunza amani ya nchi yetu katika kuleta mabadiliko na kuondokana na mgawanyiko.
Vile vile alizitaka Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kuwachunguza watendaji wake wanaokiuka sheria na taratibu za utendaji na baadaye kuweza kuwawajibisha. Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo teule Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka alisema kuna haja ya kuwatengea maeneo yaliyopimwa wafugaji na wakulima ili kuepusha vurugu kwa jamii hizo mbili.
“Naiomba serikali iweze kushughulikia suali hili la wafugaji na wakulima ili kuepukana na migogoro inayojitokeza mara kwa mara katika maeneo hayo” alisema Ole Sendeka.
No comments:
Post a Comment