TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA YAENDESHA MAFUNZO YA SIKU MBILI KWA KAMATI ZA MAADILI ZA MIKOA YA RUKWA KATAVI

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Jaji Kakusulo Sambo
akisoma
hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo mapema leo tarehe 12 Februari 2015.
Mafunzo hayo ya siku mbili yanayoshirikisha Mikoa ya Rukwa na Katavi
yanafanyika Mkoani Rukwa. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella
Manyanya na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Ibrahim Msengi.

Jaji wa Mhakama Kuu ambae pia ni Mkuu wa Chuo cha Mahakama Lushoto Jaji
Ferdinand
Wambali akiendesha mafunzo hayo ambayo yameanza leo tarehe 12 Februari
na yatamalizika kesho tarehe 13 Februari 2015 katika ukumbi wa Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (RDC).

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Ibrahim Msengi akitoa shukurani za Mikoa ya
Rukwa
na Katavi kwa kuletewa mafunzo hayo ambayo ni muhimu kwa Kamati za
maadili za Mikoa hiyo katika utekelezaji wa majukumu yake ya siku.

Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu
Iddi Kimanta (wa kwanza) na Katibu Tawala Wilaya Kalambo Bi Mapinduzi
Severian ambao ni Wajumbe wa Kamati ya maadili Mkoa wa Rukwa
wakifuatilia mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment