Header Ads

SERIKALI YAJIPANGA KUTUMIA NGUZO ZA ZEGE KUSAMBAZA UMEME


Wataalam wa Sekta ya Umeme kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Shirika la Umeme nchiniTanesco), wakiongozwa na Kamishna Msaidizi wa Umeme Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza kushoto), wakiwa katika mazungumzo na wawakilishi wa Kampuni ya Sunshine Group Ltd (Kulia). Mazungumzo yalifanyika hivi karibuni Makao Makuu ya Wizara, jijini Dar es Salaam na yalihusu uanzishwaji wa Kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme za zege kwa ajili ya kusambaza umeme nchini.
 Ujumbe kutoka Kampuni ya Sunshine Group Ltd, ukiwa katika mazungumzo na wataalam wa Sekta ya Umeme kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Shirika la Umeme nchini – Tanesco (hawapo pichani). Kampuni hiyo iliwasilisha mapendekezo (proposal) ya kuanzisha Kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme za zege kwa ajili ya matumizi ya hapa nchini.

No comments:

Powered by Blogger.