Picha Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini -Wizara ya Ujenzi :Makamu wa Rais Dr Gharib Bilal akagua mzani wa Kisasa wa Vigwaza na kufungua barabara ya Msoga - Msolwa km 10
Mzani
wa Kisasa wa Vigwaza kama unavyoonekana. Mzani huu utapima magari kwa
haraka zaidi kwa muda wa sekunde 30 kwa kila gari tofauti na mizani ya
sasa inayotumia dakika moja na nusu mpaka mbili.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kulia akisalimiana na Waziri wa Elimu
ambaye pia ni Mbunge wa Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa kabla ya ukaguzi
wa Mzani wa Vigwaza.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed
Gharib Bilal akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli pamoja na
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete, akikata utepe kuashiria ufunguzi
wa barabara ya Msoga-Msolwa km 10 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha
lami.
Makamu
wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akizungumza mara baada ya
kutoa pole kwa wananchi wa kijiji cha Msoga, Chalinze mkoani Pwani
walioathirika na kimbunga kikali kilichosababisha kubomoka kwa nyumba
zaidi ya 40 katika kijiji hicho pekee.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kushoto akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib
Bilal kuhusu Mzani wa kisasa wa Vigwaza uliopo Mkoani Pwani ambao
umekamilika kwa asilimia 99.8.
No comments:
Post a Comment