Mwakilishi wa jimbo la Magomeni, Salmin Awadhi Salmin amefariki dunia ghafla jana mchana akiwa mkutanoni katika ofisi kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar.

Mwakilishi wa jimbo la Magomeni, Salmin Awadhi Salmin (pichani) amefariki
dunia ghafla jana mchana akiwa mkutanoni katika ofisi kuu ya Chama cha Mapinduzi
CCM Kisiwandui Zanzibar.
Salmin Awadh ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mnadhimu wa wajumbe wa CCM Baraza la
Wawakilishi Zanzibar amefariki wakati akihudhuria vikao vya chama.
Marehemu Awadh alikimbizwa kwa matibabu Hospitali ya Mnazi Mmoja, Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment