MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AKABIDHI KATIBA PENDEKEZWA KWA WILAYA ZOTE MKOANI RUKWA LEO
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kulia akimkabidhi Katibu Tawala
Wilaya ya Kalambo Bi. Mapinduzi Severian Katiba pendekezwa leo tarehe 14
Februari 2015 kwa niaba ya wananchi wa Wilaya hiyo ambao watapata fursa
ya kuiona na kuisoma kwa ajili ya kuipigia kura ya maoni mwezi Aprili
mwaka huu.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akimuonyesha muimbaji wa kikundi
cha ngoma za asili ya Kanondo Katiba pendekezwa katika hafla fupi ya
kukabidhi Katiba hiyo iliyofanyika katika Wilaya ya Kalambo.
\Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akimuonyesha Ndugu Mulele Mulenda
Mwanaukawa aliyeshiriki hafla hiyo fupi ya kukabidhi Katiba pendekezwa
kwa niaba ya Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Kalambo sehemu ya vifungu
vya katiba pendekezwa ambavyo vipo na vilikuwepo kwenye rasimu ya Katiba
ya Jaji J. Warioba ambpo ni kinyume na inavyodaiwa na UKAWA kuwa
vimechakachuliwa.
Sehemu ya washiriki wa hafla hiyo, Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na wananchi wa Wilaya
ya Kalambo muda mfupi baada ya kukabidhi Katiba pendekezwa. Aliwataka
wananchi hao kujitokeza kwa wingi mwezi April kwa ajili ya kuipigia kura
katiba hiyo na kutopotoshwa kwa namna yeyote ile na watu wasioitakia
mema nchi yao. Alisema kuwa katiba hiyo ni nzuri kwani imegusa maslahi
ya watanzania wote na ustawi wa taifa kwa ujumla.
Baadhi ya wananchi wakionekana kujifunika na mwanvuli kufuatia mvua iliyokua ikinyesha mwishoni mwa hafla hiyo.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa)

No comments:
Post a Comment