MAKALA YA SHERIA: NAMNA YA KUWASHITAK ASKARI WANAOWABAMBIKIZA KESI RAIA
Na Bashir Yakub.
Hapa
kwetu Tanzania habari ya kubambakiziana kesi ni kama mtindo. Mara
nyingi matendo haya yamekuwa yakifanywa na watu wenye uwezo kifedha
dhidi ya wasio na fedha pia kati ya maofisa wa polisi na raia. Mtu
kwasababu ana pesa au cheo anaweza kuamua kumfungulia yeyote mashtaka.
Watu wengi wako magerezani kwa kubambikizwa kesi, hili wala sio siri
tena. Siseme walio mahabusu, hao nao hawana idadi. Inasikitisha mno. Ni
wazi kuwa wengi wao wamefikia huko aidha kwa kusingiziwa kosa na askari
au mtu mwenye cheo au fedha. Lakini zaidi wametoka mikononi mwa askari
kwakuwa hata huyo mwenye cheo au fedha hawezi kumbambikizia mtu kesi
bila kupitia kwa askari. Kwahiyo askari ndio tatizo kubwa katika
hili.
1.NINI MAANA YA KUBAMBIKIZWA KESI.
Kubambikizwa
kesi au kumshtaki mtu kwa hila maana yake ni kumfungulia mtu kesi ya
jinai bila mafanikio , na bila sababu za msingi za kufanya hivyo na
mtu huyo akapata athari zozote kutokana na kumfungulia kesi hiyo. Athari
ni pamoja na kupotezewa muda, gharama, usumbufu, kudhalilishwa, kupata
hasara kibiashara au kikazi kutokana na kushikiliwa na kila kitu
ambacho kimekuwa kama matokeo ya kusingiziwa kesi ni athari kwa maana
hii.
2. SABABU ZA KUWABAMBIKIZA WATU KESI.
Sababu
za kumuuzia mtu kesi huwa ni nyingi. Ni nyingi kutokana na kuwa
kila aliyebambikizwa kesi huwa kuna mgogoro nyuma uliosababisha jambo
hilo na migogoro kawaida inatofautiana. Pamoja na hayo sababu kuu
za kubambikizia mtu kesi huwa ni kwa ajili ya kumkomoa au kulipiza
kisasi kutokana na chuki zilizotokana na mgogoro kama nilivyosema.
3. WELEDI WA ASKARI WETU NA KUWABAMBIKIZIA RAIA KESI.
Wakati
mwingine askari wetu huwabambikizia watu kesi katika mazingira
ya kushangaza kabisa. Askari anaweza kumbambikizia raia kesi
kwasababu tu raia amehoji jambo fulani. Kwa mfano mtu anaweza
kumuuliza askari nioneshe kitambulisho chako kabla hujanikamata.
Utasikia askari akimwambia mtu unajifanya mjuaji tutaona, mara
unanifundisha kazi utanitambua n.k. Eti mazimgira kama hayo kwa askari
wetu utakuwa tayari ni mgogoro na mtu atapofikishwa kituoni basi ni
rahisi kupewa kesi ambayo si yake ilimradi tu askari aoneshe kuwa
aliposema utanitambua, utaona alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo
kweli.

No comments:
Post a Comment