kiwanda kikubwa cha A to Z cha Arusha,Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni IPP Reginald Mengi Wamsaidia Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa jimboni kwake,wamchangia shule iliyoungua
Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa
akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule sekondari ya wavulana ya
Engutoto wilayani Monduli wakati alipotembelea leo.Lowassa ambaye alirejelea
kauli yake ya kwamba yeye si tajiri bali ni tajiri wa marafiki, alichangia
shilingi milioni tatu kwa ajili ya sare za shule kwa wanafunzi ambao nguo zao
ziliteketea.Aidha mwenyekiti mtendaji wa makampuni IPP amechangia shilingi
milioni 25 kwa ajili ya vitanda.
Mmiliki wa kiwanda kikubwa cha A to Z cha Arusha,Anoji Shah
(aliesimama) akiwaeleza wanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Engutoto
wilayani Monduli umuhimu wa elimu na pia kutangaza msaada wa enzi wa mabweni
yote mawili yaliyoteketezwa kwa moto wiki mbili zilizopita.
No comments:
Post a Comment