Taasisi ya WAMA Foundation imefanikiwa kupanua fursa za elimu kwa mtoto wa kike kwa mwaka 2014.

Hayo
yamesemwa na Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma
Kikwete wakati Akiongea na wenza wa mabalozi kutoka nchi mbalimbali katika ghafla
fupi ya kuukaribisha mwaka mpya 2015 iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam,
Mama
Salma alisema kuwa baadhi ya mafanikio yaliyofikiwa na Taasisi ya WAMA ni
kukamilika kwa sekondari ya WAMA Sharaf
katika Manispaa ya Lindi.
“Ninayo
furaha kuwataarifu kwamba ujenzi wa shule ya sekondari ya WAMA Sharaf
umekamilika, shule ambayo itaongeza idadi ya wasichana wanaofaidika na WAMA”
Alisema Mama Salma.
Aidha,
aliitaja Shule ya Sekondari ya Wasichana ya WAMA Nakayama kuwa sehemu ya
mafanikio ya Tasisi hiyo ambayo ina idadi ya wanafaunzi zaidi ya 400 na
inatarajia kuchukua wanafunzi 90 mwaka 2015, ambao ni yatima na wanaotoka
kwenye mazingira magumu.
Akiongelea
kuhusu mafanikio mengine Mama Salma alisema ni pamoja na kuimarisha afya ya
mama wajawazito na watoto ili kupunguza vifo, kupunguza mimba za utotoni, na
kupunguza kasi ya maambukizi ya HIV toka kwa mama kwenda kwa mtoto
Mama
Salma aliwashukuru wadau wote wanaofanya kazi kwa kushirikiana na WAMA wakiwemo
Mashirika yasiyo ya Serikali kwa misaada na kuwaomba waendelee kushirikiana ili
kutoa mabadiliko chanya katika jamii husika.
Aidha,
kwa niaba ya wenza wa mabalozi waliohudhuria ghafla hiyo, Mke wa kiongozi wa
mabalozi nchini Bi Celine Mpango alimpongeza Mama Salma Kikwete kwa juhudi
anazofanya katika kumkomboa mtoto wa kike na mwanamke kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment