SOMA TAARIFA YA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MAANDALIZI YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva
akizunguza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya tume ya
uchaguzi jijini Dar es salaam wakati alipozungumzia maandalizi ya
uboreshaji wa daftari la wapiga kura, kura ya maoni ya Katiba mpya na
uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu, kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya
Uchaguzi Bw. Julius Mh.Julius Mallaba.

Baadhi ya waadishi wa habari wakiwa katika kutano huo.
----

Ndugu Waandishi wa Habari,
Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Watendaji wa Tume,
Mabibi na Mabwana.
Kwa
niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, napenda kuchukua fursa hii
kuwakaribisheni kwa mara nyingine katika Mkutano huu. Nawashukuru
kwamba, pamoja na majukumu mengi mliyo nayo, mmeweza kuupa umuhimu wa
pekee mkutano wetu huu na kuhudhuria kwa wingi. Kwa niaba ya Tume ya
Taifa ya Uchaguzi, nasema Ahsanteni na Karibuni sana.
Katika
mkutano huu, Tume inalenga kutoa taarifa kuhusu tathmini ya utekelezaji
wa zoezi la majaribio ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
(Pilot Registration) kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR)
zoezi ambalo lilikamilika wiki iliyopita.
Ndugu Wanahabari,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi, imepewa jukumu la kisheria Kuandikisha
Wapiga Kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuliboresha
Daftari hilo kwa ajili ya Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Wabunge na Madiwani. Kwa mujibu wa Sheria ya Kura ya Maoni,
Daftari hili la Kudumu pia litatumika katika Kura ya Maoni kuhusu Katiba
Inayopendekezwa.
Ndugu
Wanahabari; mtakumbuka kuwa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa katika
mchakato wa Maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
kwa kutumia Teknolojia Mpya ya ”Biometric Voter Registration” (BVR) na
mara kwa mara imekuwa ikiomba kukutana nanyi ili kuwapa taarifa kuhusu
hatua mbalimbali ambazo Tume imekuwa ikizipitia.
Kwa
kuwa Uboreshaji huu ulihusisha matumizi ya vifaa vya teknolojia ya
kisasa, vifaa ambavyo vilikuwa havijawahi kutumika katika Uboreshaji
nchini, tuliona si vyema kuagiza vifaa vingi kabla ya kuvifanyia
majaribio. Zoezi la majaribio lilifanyika ili kuwa na uhakika kuwa vifaa
hivi vya Biometric Registration vina uwezo wa kuandikisha Wapiga Kura
katika mazingira ya nchi yetu.
Zoezi
hili liliangalia uwezo wa watendaji kutumia BVR katika uandikishaji na
pia uwezo wa vyombo vyenyewe katika Software na Hardware kwenye
uandikishaji. Katika zoezi hili tuliangalia changamoto zilizojitokeza
ili kuzipatia ufumbuzi kabla ya kuanza Zoezi halisi la Uandikishaji wa
nchi nzima.
Ndugu Wanahabari,
Kama nilivyosema, Tume inakutana nanyi ili kuwapa taarifa kuhusu
Tathmini ya Utekelezaji wa zoezi la Majaribio la Uboreshaji wa Daftari
la Kudumu la Wapiga Kura lililofanyika kwa siku saba (7) katika Kata za
Bunju na Mbweni katika Jimbo la Kawe, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar
es salaam; Kata za Ifakara, Kakingiuka, Ipangala, Mlabani na Viwanja
Sitini katika Jimbo la Kilombero Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero,
mkoani Morogoro; na Kata za Ikuba, Usevya na Kibaoni katika Jimbo la
Katavi, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
Tume
kwa namna ya pekee, inawashukuru sana Waandishi wa Habari kwa
kujitokeza na kufuatilia zoezi hili la majaribio ya uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Waandishi wa Habari wamesaidia sana
katika kuhamasisha Wananchi wa Majimbo husika kujitokeza kwa wingi
kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Vilevile,
Waandishi wa Habari wamesidia katika kutoa taarifa za maendeleo ya zoezi
hili kitu ambacho kimesaidia kufanikisha zoezi hili.
Jumla
ya BVR Kits 250 zilitumika katika Uboreshaji huo kwa mgawanyo ufuatao:-
Halmashauri ya Kilombero BVR Kits 80, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele
BVR Kits 80 na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni BVR Kits 90. Vituo
katika Kata zote vilikuwa vinafunguliwa saa 2.00 asubuhi na kufungwa saa
12.00 jioni
Ndugu Waandishi wa Habari,
Tume inapenda kuwafahamisha kuwa zoezi hilo la Majaribio ya
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika majimbo matatu
yaliyotajwa limefanyika na kukamilika kwa mafanikio makubwa. Changamoto
zilizojitokeza hapa na pale zimetusaidia kupata ufumbuzi ambao
utatusaidia wakati wa Uandikishaji wenyewe nchi nzima. Tunasema
mafanikio makubwa kwa sababu matokeo ya jumla yanaonyesha kuwa idadi ya
wapiga kura waliojitokeza kujiandikisha ilikuwa kubwa na kuvuka malengo
ya waliokadiriwa kuandikishwa.
No comments:
Post a Comment