Header Ads

Soma Taarifa Kuhusu Waliochaguliwa Kwenye Ufadhili wa Serikali ya Oman


Kamati ya pamoja inayoratibu program ya “Oman Academic Fellowship” (OAF)
inayodhaminiwa na Falme ya Oman, inapenda kutangaza kwamba waombaji wafuataowamekubaliwa kupata udhamini wa masomo kwa ngazi za Masters na PhD kwa mwaka 2014/2015 katika masomo walioomba kama inavyoonekanwa kwenye Jedwali.

Waombaji hawa wanatakiwa wafuate maelekezo yafuatayo:
  • Wawasilishe kopi za vyeti na vyeti vyao vya asili kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Chuo Kikuu cha Taifa Cha Zanzibar, kwa ajili ya kuthibitishwa
  • Watafute vyuo kwa ajili ya masomo yao. Muombaji anaweza kuomba Chuo chochote ulimwenguni ambacho kimo katika vyuo 200 bora ulimwenguni katika mfumo wa Shanghai Ranking inayoparikanwa katika tovuti: www.shanghairanking.com
  • Wafanye mitihani ya lugha ya Kiingereza na wapate alama kama ilivyotangazwa
Kwa taarifa zaidi, waombaji waliokubaliwa wawasiliane na Naibu Makamu Mkuu – Taaluma, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Tunguu Campus. Au watumie anuani za barua pepe zifuatazo: dvcacademic@suza.ac.tz au haji.mwevura@suza.ac.tz

No comments:

Powered by Blogger.