RIDHIWANI KIKWETE AAPA KUPAMBANA NA MATAPELI WA ARDHI JIMBO LA CHALINZE
Mbunge
wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete,akihutubia katika mkutano wa
hadhara katika Kijiji cha Fukayosi, Kata ya Fukayosi, wakati wa ziara ya
kikazi pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge miezi
sita iliyopita.Ridhiwani kutoruhusu hata kipande cha heka moja kuporwa
na matapeli katika jimbo lake la Chalinze.PICHA ZOTE NA RICHARD
MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Kijana Salumu Khamis akiuliza swali mbele ya Mbunge Ridhiwani Kikwete kuhusu tatizo la maji katika Kijiji cha Fukayosi
Mkuu
wa Miradi wa Mkoa wa Pwani wa Tanesco, Leo Mwakatobe, akielezea jinsi
umeme utakavyosambazwa katika Kijiji cha Fukayosi na vijiji vingine
Jimbo la Chalinze.
Mwenyekiti
mpya wa Serikali ya Kijiji cha Fukayosi, Salum Mkwecha akimshukuru
mbunge kwa ahadi mbalimbali alizozitoa katika miradi mbalimbali katika
kijiji hicho.
Ridhiwani
akibadilishana mawazo na mmoja wa watawa baada ya kumalizika kwa
mkutano katika Kijiji cha Fukayosi Jimbo la Chalinze.
Mwenyekiti
mstaafu wa Kata ya Fukayosi,Adam Masoud akimuomba Mbunge Ridhiwani
kuhikisha anaweka miundombinu ya barabara na maji na masuala ya afya
katika Kijiji cha Mkenge,wakati wa ziara yake katika Kata ya Fukayosi ya
kuwashukuru kwa kumchagua pamoja na kusikiliza kero za wananchi na
kuangalia jinsi ya kuzitafutia ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment