Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju Akaribishwa Rasmi Wizara ya Katiba na Sheria

Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju (kushoto) akikaribishwa Wizara ya
Katiba na Sheria kwa shada la maua kutoka kwa mtumishi wa Wizara Bi.
Christina Jenga jana (Jumatano, Januari 7, 2015) jijini Dar es Salaam
huku Katibu Mkuu wa Wizara Bi. Maimuna Tarishi akishuhudia. Bw. Masaju
alifika Wizarani kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe na Rais Jakaya
Kikwete ili kubadilishana mawazo na viongozi na watumishi wa Wizara.

Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju akipokewa na watumishi wa Wizara ya
Katiba na Sheria jana(Jumatano, Januari 7, 2015) wakati alipofika
Wizarani hapo kukutana na viongozi na watumishi ili kubadilishana
mawazo.

Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju (kushoto) akibadilishana mawazo na
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro jana(Jumatano, Januari
7, 2015) wakati alipofika Wizarani kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe na
Rais jakaya Kikwete hivi karibuni.
---
Na Mwandishi Wetu
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju amewakumbusha watumishi wa umma
katika sekta ya sheria kufanya kazi kwa ushirikiano na uzalendo ili
kulinda maslahi ya taifa.
Bw.
Masaju, ambaye ameteuliwa na kuapishwa hivi karibuni na Rais Jakaya
Kikwete kushika wadhifa huo, amefafanua kuwa watumishi wa umma
wanapozingatia uzalendo katika utendaji wao, wanapata nguvu ya kusimama
na kukemea maovu.
No comments:
Post a Comment