WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO APATA MAPOKEZI MAKUBWA WILAYANI KISHAPU MKOANI SHINYANGA. AITWA “MZEE WA NGUZO”
Wakazi
wa Kata ya Bubiki wilayani Kishapu wakimpokea kwa shangwe Waziri wa
Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo mara alipowasili wilayani
hapo huku wakiwa na mabango yaliyosomeka “ Profesa wa Kweli, Nchi sasa
inang’aa vijijini, Wewe ni Jembe”.
Mmoja
wa wakinamama kutoka kata ya Igubi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga
akimfunga vitambaa mkononi Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo kama heshima kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kusambaza umeme
katika kata hiyo. Kata hiyo ni moja ya kata zinazonufaika na mradi wa
umeme vijijini unaotekelezwa na REA Awamu ya Pili
Mbunge
wa Kishapu Suleiman Masoud Nchambi (katikati) akijumuika na wakazi wa
Kata ya Igumbi iliyopo wilayani Kishapu kucheza ngoma ya kumpongeza
Waziri wa Nishati na Madini kwa juhudi zake za kusambaza umeme katika
kata hiyo pamoja na jimbo lake.
No comments:
Post a Comment