Header Ads

MBUNGE WA MOROGORO MJINI MH ABOOD ATOA MILION 11 KUTATUA KERO YA MAJI MKUNDI MOROGORO

 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akizindua Tawi la CCM la Wajasiriamali Bodaboda na Mama lishe lililopo Mgulu wa Ndege Kata Ya Mkundi Manispaa ya Morogoro.Mara Baada ya Kuzindua Tawi Hilo Mh Abood Aliongea na Wanachama wa Tawi Hilo Kisha Kuwaelekeza Kujiunga Kwenye Vikundi vya Wajasiriamali Yeye Atakuwa Tayari kuwawezesha Mitaji ya Kufanya Shuguli za Kujiletea Maendeleo.

 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwa Meza Kuu Sambamba na Katibu wa CCM Kata Ya Mkundi tayari Kusikiliza Kero zinazowakabili wakati wa Kata hiyo,ambapo walimwambia Wanakabiliwa na Kero Kubwa ya Umeme,Maji na Barabara.

Aidha Mh Abood ametoa majibu Kuhusu Kero hizo na kusema kuwa Serikali imeiweka Kata hiyo Kwenye Bajeti ya Serikali ya Mwaka huu .Kuhusu Maji Mh Abood alitoa Shilingi Milioni 11 Kwa jili ya Kununua Vifaa vya Kuwezesha Kufikisha Maji katika eneo la Mgulu wa Ndege Kata ya Mkundi.Pia Alitoa Shilingi Milion 2 kwa ajili ya kuhakikisha barabara zote za Kata hiyo zinachongwa.
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Mgulu wa Ndege Kata ya Mkundi Jimbo la Morogoro Mjini Akisoma Risala yake Kwa Mbunge wa Jimbo Hilo Mh Aziz Abood.

No comments:

Powered by Blogger.