Header Ads

Mabingwa wa Soka Tanzania Azam Fc Kuweka Kambi Nchini Kongo



Mabingwa wa Soka nchini Tanzania Azam Fc wanatarajia Kuweka kambi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwaajili ya kucheza mechi nne za kirafiki ikiwa ni kujiandaa na mechi ya ligi ya klabu bingwa ya Afrika dhidi ya vigogo wa Sudan timu ya El-Merreikh

Jaffar Iddi, msemaji wa klabu ya Azam amesema wakiwa Congo, watacheza na timu kubwa nne na kurejea nchini Tanzania Mnamo February 4 kwaajili ya kujiandaa na kucheza Mechi na Elh-Merreikh Jijini Dar kati ya February 13, 14 na 15.

“Bado hatujajua timu tutakazocheza nazo kwa kuwa bado tupo katika mazungumzo aliongezea Jaffar”.

Ni mara ya kwanza kwa timu ya Azam kushiriki ligi ya klabu bingwa Afrika, Azam Fc inatarajia kuondoka kuelekea Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mara baada ya kumaliza kucheza mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara ambayo itachezwa January 24 dhidi ya mabingwa wa zamani Wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club.

Wakati Azam wakiwa kwenye maandalizi ya Mechi yao wapinzani wao El-Merreikh tayari washacheza mechi kadhaa za majaribio ikiwa pamoja na kutoka sare ya magoli 2 kwa 2 na Timu ya Schalke 04 inayoshiriki ligi ya Bundersliga nchini Ujerumani.
Mbali na Azam, wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano ya CAF ya vilabu ni Young Africans (Yanga), wanaotegemewa kucheza na timu ya jeshi la Botswna, BDF XI katika mechi ya awali ya kombe la shirikisho.
Kwa upande wa Zanzibar, mabingwa KMKM watakiputa na timu nyingine ngumu ya Sudan, Al Hilal katika klabu bingwa Afrika wakati katika kombe la shirikisho, Polisi watacheza na CF Mounana ya Gabon.

No comments:

Powered by Blogger.