Header Ads

Vijiji 45 mkoani Mara kupatiwa umeme


indexaWaziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa vijiji vipatavyo 45 vilivyopo katika mkoa wa Mara vinatarajiwa kuunganishiwa na huduma ya umeme kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
  Profesa Muhongo aliyasema hayo katika ziara yake ya siku sita katika mkoa wa Mara lengo likiwa ni kukagua na kuzindua miradi ya umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya pili kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini (Tanesco).
  Profesa Muhongo alisema ziara yake iliyohusisha wilaya za Musoma Vijijini, Tarime, Rorya, Bunda na Serengeti ililenga pia kubaini na kukagua mahitaji ya umeme katika wilaya hizo ili vijiji vilivyokosa umeme kwenye awamu ya pili viingizwe katika awamu nyingine ya umeme vijijini.
  Alieleza kuwa Wizara imekuwa ikisambaza umeme katika kila Mkoa na Wilaya za Tanzania kwa awamu kulingana na mahitaji na idadi ya watu katika maeneo hayo.
  Alisema kwa sasa umeme unaosambazwa upo katika awamu ya pili ambapo awamu ya tatu itakuja baada awamu ya pili kumalizika.  Alisema vipaumbele vinavyotolewa katika uunganishaji wa umeme vijijini Profesa Muhongo alitaja kuwa ni maeneo yenye huduma muhimu za kijamii kama vile mashule, vituo vya afya, makanisa, misikiti, ofisi za vijiji na kata, na sehemu zenye miradi ya maji.

No comments:

Powered by Blogger.