NDEGE YA AIR ASIA YAONEKANA CHINI YA BAHARI
Hatimaye ndege ya Indonesia ‘Air Asia’ iliyokuwa na abiria na watumishi 162 iliyotoweka tangu Jumapili(Dec.28) imepatikana ikiwa chini ya bahari karibu na kisiwa cha Borneo.
Mkuu wa idara ya utafiti na uokozi ya Indonesia, Bombang
Soelistyo amesema vikosi vya uokoaji viliokoa miili 40 katika bandari ya
eneo hilo huku juhudu za kuifikia miili mingine iliyoko ndani ya ndege
iyo zikiendelea.
Watafutaji wa ndege iyo kutoka angani waligundua kitu
kinachoonekana kama kivuli chini ya bahari ambapo walikifuatilia na
kuigundua kuwa ni ndege iyo.
Miili ilipatikana mara baada ya kugundulika kwa mabaki ya
ndege pamoja na kitu kilichoonekana kuwa kifaa cha kujiokoa baharini,
mizigo na mlango wa dharura uliopakwa rangi nyeupe na nyekundu.

Raia wa Indonesia wakilia baada ya kupewa taarifa ya kupatikana kwa ndege ya Air Asia chini ya bahari

Ndugu
waliopoteza wapendwa wao kwenye Air Asia wakilia mara baada ya kupewa
taarifa ya kupatikana kwa ndege ya Air asia chini ya bahari

Wafanyakazi wa vikosi vya uokoaji wakiifunika miili ya abiria wa Air Asia waliopatikana chini ya kina cha bahari ya java

Vikosi vya usalama na uokoaji vikiwa vimebeba miili ya abiria waliopatikana kwenye ndege ya Air Asia chini ya bahari
No comments:
Post a Comment