MAONYESHO YA KIMATAIFA YA ELIMU KUANZA DISEMBA 17-21, 2014 JIJINI DAR

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Abdulimalik Mollel, akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani)
Kampuni
ya Global Education Link (GEL) kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu
(TAMISEMI), Wizara ya Elimu na Ufundi pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya
Biashara Tanzania (Tantrade) wameandaa maonyesho ya kwanza ya kimataifa
ya elimu (TIEE) yanayotarajiwa kufanyika Disemba 17 hadi 21 mwaka huu
katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Global link Education,
Abdulmalik Mollel, alisema lengo la maonyesho hayo ni kutambulisha wadau
wa elimu kwa pamoja ili kuweza kutoa huduma ya pamoja kwa wananchi na
kuwaelimisha juu ya mambo muhimu yaliyopo katika kila sekta.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Tred), Jacqueline Mneney, akizungumza jambo.
Alisema
ushiriki wa asasi mbalimbali kwa kushirikiana na sekta binafsi utakuwa
na chachu ya mabadiliko ya elimu kwa kupitia mpango wa matokeo makubwa
sasa. Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade),
Jacqueline Mneney, alisema wakati umefika kwa Watanzania kujua umuhimu
wa maonyesho ya Elimu maana yamekuja kutatua matatizo mbali mbali
waliyokuwa wakiyapata wazazi pindi wanapokuwa wanawatafutia shule na
vyuo watoto wao.
Aidha
alisema maonyesho hayo yataleta manufaa makubwa na changamoto chanya
hasa katika kuongeza ushindani katika sekta ya elimu ambayo itasaidia
mpango wa matokeo makubwa sasa. Maonesho hayo yanatarajiwa kupata washiriki zaidi ya 500 na wananchi mbalimbali zaidi ya 350,000 kutoka ndani na nje ya nchi.
Kauli mbiu ya maonesho hayo ni ‘KUWEKA JITIHADA ZA PAMOJA KATIKA KUBORESHA MFUMO WA ELIMU TANZANIA NI NJIA THABITI YA KULETA MAENDELEO ENDELEVU KATIKA TAIFA.’
No comments:
Post a Comment