MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAAGA WATOTO WENYE MATATIZO YA MOYO KWENDA KUTIBIWA INDIA

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi zawadi mtoto, Nabil Hahya (4) kutoka Jijini Dar es Salaam,
mmoja kati ya watoto 55 wa awamu ya kwanza kati ya 104 wenye matatizo ya
ugonjwa wa Moyo wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi
ya kuwaaga watoto hao iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli
ya Serena Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mama wa motto huyo, Amina
Yahya.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Desemba 26, 2014
kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ya kuwaaga jumla ya watoto
55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, waliofadhiliwa na
Lions Club ya jijini, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto
hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.
No comments:
Post a Comment