DICOTA WAMKABIDHI BALOZI LIBERATA MULAMULA RIPOTI YAO YA DICOTA CONVENTION 2014 ILIYOFANYIKA NORTH CAROLINA
Viongozi
wa DICOTA Lunda Asmani (kushoto)na Dr. Kurwa Nyigu wakitia saini kitabu
cha wageni mara tu walipofika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
uliopo Washington, DC kuonana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamuala (hayupo pichani) na
kumkabidhi ripoti ya mkutano wa kongamano wa DICOTA uliofanyika mapema
mwezi wa Oktoba kwenye tarehe 2 mpaka 5 2014.
Viongozi
wa DICOTA Dr. Kurwa Nyigu (kushoto na Lunda Asmani(wapili toka kushoto)
wakifanya mkutano wa makabidhiano ya ripoti ya mkutano wa kongamano wa
DICOTA wa 2014 na Mhe. Liberata Mulamula akiwemo Afisa Ubalozi Switebert
Mkama(kulia) jioni ya Jumatatu Desemba 8, 2014 katika Ubalozi wa
Tanzania nchini Marekani uliopo barabara ya 22 NW, Washington, DC.
Mkutano wa makabidhiano ukiendelea
Kiongozi
wa DICOOTA Lunda Asmani akimkabidhi Mhe. Balozi Liberata Mulamula
Ripoti ya mkutano wa kongamano wa DICOTA wa 2014 uliofanyika mapama
mwezi wa Oktoba Durham, North Carolina nchini Marekani.
Kiongozi wa DICOTA Lunda Asmani akitoa maelezo kwa Mhe. Balozi Liberata Mulamula kuhusiana na ripoti hiyo.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiipitia kwa haraka haraka ripoti hiyo
Kiongozi
wa DICOTA Lunda Asmani akimkbidhi Mhe. Balozi Liberata Mulamula DVD za
mkutano wa kongamano wa DICOTA wa 2014 uliofanyika mapema mwezi Oktoba
Durham North Carolina nchini Marekani.
Kiongozi wa DICOTA Lunda Asmani akiemwelezea jambo mhe. Balozi Liberata Mulamula.
Kiongozi Lunda Asmani akiendelea kuelezea jambo huku kiongozi mwenzake Dr. Kurwa Nyigu akimsikiliza.
Afisa
Ubalozi Switebert Mkama akifuatilia mkutano wa makabidhiano wa ripoti
ya DICOTA Convention 2014 uliofanyika Durham, North Carolina mapema
mwezi wa Oktoba 2014.
---
Viongozi wa DICOTA Lunda Asmani na Dr. Kurwa Nyigu walifika jioni ya Desemba 8, 2014 ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington DC kumkabidhi Mhe. Liberata Mulamula ripoti ya mkutano wa kongamano wa DICOTA wa 2014 uliofanyika mapema mwezi Oktoka kati ya tarehe 2 mpaka 5.
Viongozi wa DICOTA Lunda Asmani na Dr. Kurwa Nyigu walifika jioni ya Desemba 8, 2014 ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington DC kumkabidhi Mhe. Liberata Mulamula ripoti ya mkutano wa kongamano wa DICOTA wa 2014 uliofanyika mapema mwezi Oktoka kati ya tarehe 2 mpaka 5.
No comments:
Post a Comment