SHEREHE ZA UN ZAFANA: TANZANIA YATAKA UTEKELEZAJI MFUKO WA GCF
Pichani juu na chini ni Mratibu Mkazi
wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimtambulisha mgeni
rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna
Tibaijuka kwa baadhi ya wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini
mara baada ya kuwasili kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya
Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo
ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akipokea heshima ya wimbo wa taifa
kabla ya kuanza rasmi kwa sherehe za maadhimisho miaka 69 ya Umoja wa
Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo
ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akikagua gwaride maalum kwenye sherehe
za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake
zilizofanyika leo jijini Dar.

Mgeni
rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna
Tibaijuka akisoma risala kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya
Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake yaliyofanyika kwenye viwanja vya
Karimjee jijini Dar.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisoma
ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kwenye sherehe za
maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika kwenye
viwanja vya Karimjee jijini Dar.
No comments:
Post a Comment