CHUO CHA TAALUMA ZA SAYANSI ZA AFYA ZANZIBAR CHAFANYA MAHAFALI YA 21,WAHITIMU 280 WATUNUKIWA STASHAHADA.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Taaluma za Afya Zanzibar Dkt. Abdalla
Ismail Kanduru akitoa tamko la kuwatunuku stashahada wahitimu wa Chuo hicho
katika Mahafali ya 21 yalifanyika Mbweni.
Wahitimu wa Chuo cha Taaluma za Afya
Zanzibar wakila kiapo cha utiifu mbele ya mgeni rasmi Balozi Seif Ali
Iddi katika mahafali ya 21 yaliyofanyika chuoni Mbweni.
Wahitimu wa fani mbali mbali wa Chuo hicho wakimsikiliza mgeni rasmi
(hayupo pichani) baada ya kuwatunuku stashahada katika mahafali ya 21.
Wageni waalikwa walioshiriki mahafali ya 21 ya Chuo cha Taaluma za Afya
Zanzibar wakifuatilia maadhimisho hayo
yaliyofanyika Chuoni, Mbweni.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimtunuku zawadi Leila Ali kwa kuwa miongoni mwa
wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika
mahafali ya Chuo cha Taaluma za Afya Mbweni Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na
wahitimu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar katika Mahafali ya 21
yaliyofanyika Chuoni Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Wa kwanza (kulia) ni
Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman na wa kwanza (kushoto) Mwenyekiti wa Baraza
la chuo hicho Dkt. Abdalla Ismail Kanduru. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
No comments:
Post a Comment