Video ya Mb Dog kuanza kuchezwa luningani wiki hii
MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Mbwana Mohamed, Mb Dog,
amesema mashabiki wake wataanza kuona video ya wimbo wake wa Mbona Umenuna
katika vituo vya luninga ndani ya wiki hii.
Mb Dog, pichani.
Video hiyo iliyoandaliwa kwa kiwango cha juu iliingizwa
katika mitandao ya kijamii, huku kwenye luninga ikianza kusambazwa wiki hii ili
kuwapa burudani mashabiki wake.
Akizungumza leo mchana, Mb Dog alisema kwamba alianza kwanza
kuingiza kwenye mitandao ya internet ili kuwapa nafasi watu wote, wakiwamo wan
je ya nchi kuitazama video hiyo.
“Hii ni video nzuri ambayo iliingia kwanza kwenye mtandao na
kuwapa fursa watu kuitazama, ambapo natarajia mashabiki wengine wataanza
kuangalia luningani wiki hii.
"Naamini mashabiki wangu wote watapata burudani ya kutosha,
ukizingatia kuwa nimefanya video nzuri inayoonyesha umahiri wangu kisanaa,”
alisema.
Mb Dog ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva wenye uwezo wa
juu wa kutunga na kuimba, ambapo wimbo wake wa kwanza uliomuibua ni Latifa na
nyinginezo.
No comments:
Post a Comment