Shiwata kugawa mashamba kwa wanachama wake
Umeamua
kutoa ofa ya kugawa shamba lake la ekari 500 lililoko Mkuranga mkoa wa
Pwani kwa wanachama wake wenye uwezo wakulima mazao mbalimbali
yatakayochangia kupunguza uhaba wa chakula nchini.
Taarifa
kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mwenyekiti wa Mtandao wa SHIWATA,
Cassim Taalib kwa vyombo vya habari inasema wanachama watakaogaiwa
shamba hilo ni wale walio hai waliolipia ada zao watapaswa kutoa sh.
200,000 kulipia ekari moja atakayopewa.
Alisema
kuratibu mpango huo SHIWATA imeitisha mkutano wa wanachama wote
Jumamosi Juni 21,2014 kwenye ukumbi wa Splendid Ilala ili kujadili mambo
mbalimbali katika kijiji cha wasanii Mkuranga ambacho mpaka sasa
kimejenga na kukabidhi nyumba 66 kwa wanachama wake kati ya 265
wanaojenga nyumba zao kwa njia ya kuchangishana.
"Ujenzi
wa nyumba za kisasa katika kijiji chetu cha Mwanzega Mkuranga chenye
ukubwa wa hekari 300 unaendelea tunatarajia kukabidhi nyumba 40 Desemba
mwaka huu katika sherehe kubwa ambayo tunatarajia kumpata mgeni rasmi
kutoka ngazi za juu" alisema Mwenyekiti.
Alisema
shiwata inawataka wanachama wote ambao hawakuwahi kwenda kuona au
kukabidhiwa viwanja au nyumba zao kutokana na sababu mbalimbali wafike
na kadi zao ofisini Ilala Bungoni Chuo cha Splendid kabla ya Jumatano
Juni 19, 2014 ili wakakabidhiwe nyumba zao na kiwanja vyao Jumamosi Juni
21, 2014 saa 2 asubuhi kwa nauli ya sh. 10,000 ya kwenda na kurudi.
Aliwatoa
wasiwasi wanachama waliokuwa wanahofia kuwekeza katika ujenzi wa nyumba
kuwa mpango wa kupimia wasanii nyumba zao ili wapate fursa ya kukopa
kutoka benki mbalimbali za hapa nchini umeanza kushirikiana na Idara ya
Ardhi ya Halmashauri ya Mkuranga ikifuatiwa na ujenzi wa barabara,
uvutaji wa umeme na uchimbaji visima vya kisasa unafanyiwa kazi.
Aliwahimiza
wanachama wanaochangia ujenzi wa nyumba zao kukamilisha michango hiyo
ili wakabidhiwe nyumba zao kukamilisha malengo ya kuwasaidia wasanii
kujikwamua kiuchumi.
Mtandao
wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) ulianzishwa mwaka 2004 na kusajiliwa na
baraza la sanaa tanzania shiwata mwaka 2005 pia imesajiliwa na brella
kwa shughuli za kiuchumi ikiwa na dira ya kuwakomboa wasanii kuwa na
maisha bora kupitia mtandao huu ifikapo mwaka 2015.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Ofisa Habari wa SHIWATA, Peter Mwenda 0715/0752 222677.
No comments:
Post a Comment