Nigeria na Iran ni sare tasa
Timu
ya Iran na Nigeria zilitoka sare ya suluhu bin suluhu , katika mechi yao
ya kundi F huko Curitiba, kwenye fainali ya kombe la dunia siku ya
Jumatatu.
Timu hiyo ya Carlos Queiroz ilionekana kuwa ngumu kushindwa tangu mwanzoni.
Super
Eagles ya Nigeria,ambao walikua na rekodi nzuri katika michuano ya
kufuzu kwa kombe la dunia walishindwa kupenya safu ya ulinzi ya Iran.
Hii ilikua sare ya kwanza tasa katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2014.
Timu zote mbili zilijaribu kupata nafasi ya kufunga bao lakini hakuna iliyofaulu.
Iran ilipoteza nafasi ya kufunga bao pale ambapo kipa wa Nigeria, Vincent Enyeama alipouzuia mkwaju wake Reza Ghoochannejad.
Mabingwa hao wa bara Afrika mwaka 2013, walitarajiwa kushinda mchuano huo lakini timu ya Iran iliwapatia changamoto si haba.
Matokeo
haya yanaipa timu ya Argentina uongozi wa kundi hilo baada ya kuishinda
timu ya Bosnia-Herzegovina, 2-1, siku ya Jumapili.
Timu
ya Iran itakutana na Argentina siku ya Jumamosi, huko Belo Horizonte,
nayo Nigeria kuiandaa kukabiliana dhidi ya Bosnia kule Cuiaba.
Nigeria ilimiliki mchuano huo katika muda wote wa dakika 90, lakini hawakufaulu kuwashinda wa Irani.
Mkwaju wake Ghoochannejad na ule wa Ahmed Musa ndizo zilizokua nafasi nzuri za kufunga bao katika kipindi cha kwanza.
Katika kipindi cha pili, Shola Ameobi alizuiwa mara mbili na mlinzi wa Iran, Mehrdad Poolani.
Victor
Moses ndiye aliyepata nafasi ya kwanza ya Nigeria kupata uongozi lakini
mkwaju wake hafifu ulikamatwa na kipa wa Iran Reza Haghighi.
Kipa
wa Iran Haghighi, asiye na uzoefu mkubwa katika mechi za kimataifa
alionekana kutishika kila wakati washambulizi wa Super Eagles
waliposhambulia lango lake na aliponea katika dakika ya saba kutokana na
mkwaju wa kona.
Kenneth
Omeruo alitia mpira wavuni lakini refa tayari alikua ameshapuliza
kipenga kuonyesha kuwa kipa, Haghighi alikua amechezewa visivyo na John
Obi Mikel.
Emmanuel Emenike alijaribu katika upande wa kushoto, lakini Pejman Montazeri alikua kizuizi katika upande huo pia.
Katika kipindi cha pili, Iran ilianza kuonyesha kujiamini na kuanzisha mashambulizi dhidi ya lango la Nigeria.
Mchuano huu ulielekea kuonekana kuwa hafifu na hakuna timu iliyoonyesha ukakamavu wa kuchuana na Argentina ama Bosnia.
Shola
Ameobi aliingia katika nafasi yake Victor Moses katika dakika ya 52 na
akaja karibu kuipatia Nigeria bao la kwanza baada ya kupewa pasi na
Ramon Azeez.
Nigeria tena walikaribia kupata bao katika dakika za mwisho kupitia kwake Ogenyi Onazi.
Hata hivo mchuano huo ulitimia kuisha kwa sare tasa .Chanzo BBC Swahili
No comments:
Post a Comment