MAKAMU MWENYEKITI WA CCM (BARA) PHILIP MANGULA AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA CHINA LI YUANCHAO
Makamu Mwenyekiti
wa CCM Ndugu Philip Mangula akimkabidhi zawadi Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Watu wa China Li Yuanchao mara baada ya kumaliza mkutano .
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao akionyesha zawadi aliyopewa na
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula mara baada ya
kumaliza mkutano baina ya viongozi wawili.
Viongozi wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao(hayupo pichani) kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao(hayupo pichani) kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China Nchini Tanzania Lu Youqing akifafanua jambo wakati wa
Semina ya Ujamaa iliyohusisha CCM na CPC kwenye Hotel ya Serena jijini
Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti
wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula akizungumza wakati wa Semina
inayohusu Umuhimu wa Ujamaa na Kukua kwa Uchumi,wengine pichani(kushoto)
ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Abdala Bulembo ,Mwakamu Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana CCM Mboni Mhita ,Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM
Ndugu Sixtus Mapunda ,Profesa Max Muya ,na Makwaia wa Kuhenga.
Mr Ma Zhongji
kutoka Ubalozi wa China akisaidia kutafsiri wakati wa Semina ya Ujamaa
iliyohusisha CCM na CPC iliyofanyika kwenye Hotel ya Serena jijini Dar
es Salaam.
Baadhi ya Maafisa
kutoka CCM Makao Makuu wakifuatilia kwa makini Semina inayohusu Umuhimu
wa Ujamaa katika Kukua kwa Uchumi iliyofanyika katika ukumbi wa
Kivukoni,Serena Hotel Dar es Salam.
Mheshimiwa
Kingunge Ngombale Mwiru akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Hotel
ya Serena jijini Dar Es Salaam na kuwaeleza kuwa Watu wanajenga Ujamaa
wenyewe haujengwi na Viongozi peke yao.
Makamu Mwenyekiti
wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula akizungumza na Waandishi wa Habari
mara baada ya kukamilika kwa Semina inayohusu Ujamaa iliyofanyika kwenye
Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo Mangula liwaeleza
waandishi hao kuwa Ujamaa unatakiwa Ueleweke,Utekelezwe na
Uendelezwe,Semina hiyo iliwahusisha vyama vya CCM na CPC kutoka China.
No comments:
Post a Comment