RAIA WAWILI WA ROMANIA KOTINI KWA KUIHUJUMU TCRA
Na Mwene Said wa Blogu ya Jamii, Mahakamani
WATU
wawili raia wa Romania wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi
ikiwemo udanganyifu,kutumia kadi zisizosajiliwa, kuingiza nchini na
kutumia mitambo ya simu bila kibali, kutoa huduma ya mawasiliano ya
kimataifa bila kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na
kuisababishia hasara ya Sh. Bilioni 2.1 Mamlaya ya Mawasiano Tanzania
(TCRA).
Washtakiwa
hao ni, Meneja wa Kampuni ya Razvan Pimtilie (47) na Robart Kraus (27)
wakazi wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam na walisomewa mashitaka
yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mfawidhi, Isaya Arufani.
Upande
wa Jamhuri uliongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka
akisaidiana na Mwanasheria Mkuu wa TCRA, Joannes Karungura na Inspekta
wa Polisi, Jackson Kinunda.
Kweka
alidai kuwa alidai shitaka la kwanza, kati ya Aprili na Mei, mwaka huu
huko Raha Data Centre, eneo la Banda la Ngozi, Wilaya ya Ilala jijini
Dar es Salaam, bila halali na kwa makusudi washtakiwa wakiwa na nia ya
kukwepa malipo halali walitoa huduma ya mawasiliano ya kimataifa bila
leseni ya TCRA.
Shitaka
la pili, ilidaiwa kuwa siku na tarehe za tukio la kwanza, washtakiwa
walitoa huduma za simu za kimataifa bila kuwa na leseni ya TCRA.
Upande
huo wa Jamhuri uliendelea kudai kuwa, shitaka la tatu, siku na tarehe
isiyofahamika washtakiwa waliingiza nchini mitambo ya elektroniki bila
leseni ya TCRA.
Wakili
huyo Mwandamizi alidai katika shitaka la nne kuwa, siku na mahali
pasipofahamika jijini Dar es Salaam, washtakiwa waliingiza nchini
mitambo ya elektroniki bila leseni ya TCRA.
Katika
shitaka la tano, ilidaiwa kati ya Aprili na Mei, mwaka huu huko Banda
la Ngozi, jijini, kwa nia ovu na kwa makusudi, washtakiwa alitumia kadi
za simu zenye namba nne tofauti zisizokuwakuwa na usajili wa TCRA.
Ilidaiwa
katika shitaka la sita, Aprili mwaka huu jijini Dar es Salaam,
mshtakiwa wa kwanza (Pintilie), akiwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Xplora
Ltd, alisajili namba za simu mbili tofauti kutoka Kampuni ya Zantel (T)
Ltd na kuzihamishia Global COM bila leseni.
Kweka
alidai katika shitaka la saba, kwamba kati ya Aprili na Mei, mwaka huu
huko Banda la Ngozi, jijini, washtakiwa wakiwa hawana leseni ya
kuwaruhusu kufanya huduma za mawasiliano alichepusha simu za kimataifa
na kuisababishia Serikali na TCRA hasara ya Sh. 2,109,888,000.
Kwa
mujibu wa sheria ya uhujumu uchumi, washtakiwa hawakutakiwa kujibu
chochote, kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za
uhujumu uchumi hadi upelelezi utakapokamilika kesi hiyo itahamishiwa
Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Hakimu Arufani alisema kesi hiyo itatajwa Mei 27, mwaka huu na washtakiwa warudishwe rumande.

No comments:
Post a Comment