PICHA:KIMBUNGA CHA ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM ABDURAHMAN KINANA CHATUA IKUNGI,ALIYEKUA KIONGOZI WA CHADEMA ISMAIL GWAU ATUPILIA MBALI KADI YA CHADEMA NA KUJIUNGA NA CCM MBELE YA UMATI MKUBWA WA WATU

Aliyekuwa
kiongozi wa Chadema, Ismail Gwau, akitupilia mbali bendera ya CHADEMA
mara baada ya kutangaza kujiunga na chama cha CCM,katika Mkutano huo wa
hadhara.

Ismail Gwau, akionyesha kadi mpya ya CCM mbele ya Kinana na kuashiria kujiunga rasmi na CCM,Ikungi mjini.

Wananchi wa Ikungi mjini wakila kiapo cha CCM.

Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara
ulofanyika katika Kijiji cha Makiungu, wilayani Ikingu, Jimbo la
Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu wa Chadema. Katibu Mkuu wa CCM
aliwataka wananchi hao wafikirie zaidi kuhusu maendeleo ya jimbo lao na
kuacha kuamini maneno ya viongozi wao wanaowazuia kuchangia maendeleo ya jimbo lao.

Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnaye akihutubia wakazi wa Makiungu, tarafa ya
Mungaa na kuwaambia wananchi hao wakati umefika wa kuwaomndoa viongozi
ambao wanawazuia wananchi kuchangia maendeleo yao.
No comments:
Post a Comment