Header Ads

Picha na Taarifa Kutoka Wizara ya katiba na Sheria: Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP) inatarajia kutoa mafunzo kwa Waandishi wa Sheria kwa lengo la kuwaongezea uwezo wa kuandaa miswada katika lugha ya kiswahili – lugha ambayo inatumiwa na watanzania wengi.


   Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Jasmine Kairuki (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP) Bw. Philippe Poinsot alipomtembelea Naibu Waziri ofisini kwake, Mtaa wa Mkwepu, jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Mei 19, 2014). Kulia ni Naibu wake anayeshughulikia Programu Bi. Mandisa Mashologu
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Jasmine Kairuki akiagana na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP) Bi. Mandisa Mashologu (kulia) alipomtembelea Naibu Waziri ofisini kwake, Mtaa wa Mkwepu, jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Mei 19, 2014). Katikati ni Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Bw. Philippe Poinsot.Picha na Wizara ya katiba na Sheria
-- 
Na Mwandishi Wetu

Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP) inatarajia kutoa mafunzo kwa Waandishi wa Sheria kwa lengo la kuwaongezea uwezo wa kuandaa miswada katika lugha ya kiswahili – lugha ambayo inatumiwa na watanzania wengi.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Jasmine Kairuki amemwambia Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Bw. Philippe Poinsot kuwa kwa sasa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inatekeleza mkakati wa kuandaa miswada yote inayosilishwa Bungeni katika lugha mbili, Kiingereza na Kiswahili ili kuwawezesha wananchi wengi kuisoma.

No comments:

Powered by Blogger.