MKUTANO WA CCM ZANZIBAR WAFANA, WANA UKAWA WACHANWACHANWA KWA UROHO WA MADARAKA WA KUTAKA SERIKALI TATU NA KUUVUNJA MUUNGANO NA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
Mama Fatma Karume akihutubia katika mkutano huo na kukemea Ukawa
wanaotaka kuuvunja Muungano kwa kutaka Serikali Tatu katika mabadiliko
ya Katiba mpya.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrhman Kinana akimpongeza Mjane wa Hayati Abeid Amani Karume, kwa hotuba yake nzuri katika mkutano huo.
Wananchi wakishangilia katika mkutano huo hasa baada ya Mjumbe wa NEC,
Mohamed Seif Khatib kumuelezea Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad
kuwa na tabia ya kinyonga kuhusu suala la Muungano, ambapo awali
alikuwa muuminji Muungano wa Serikali tatu, mara wa mkataba na sasa
anataka Serikali tau
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akimpongeza Mohamed Seif Khatibu kwa hotuba yake nzuri/
Mjumbe wa Bunge la Katiba, Hamza Hassan Juma akielezea kwenye mkutano
huo kuhusu mambo mbalimbali yaliyokubaliwa kuwekwa kwenye Katiba Mpya
ili kupunguza kero mbalimbali za wazanzibari kwenye Muungano.
Mjumbe wa Bunge la Katiba, Steven Wassira akiwaeleza wana Ukawa kuwa
hawawezi kutenganisha Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar kama ilivyo
uhusiano wa Uhuru wa Tanganyika na Muungano
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Ali Seif Idd akihutubia
katika mkutano huo na kupendekeza UKAWA kufutwa kwa vile haina uhalali
wowote akidai kuwa si chama kwani haina usajili. Alisema kuwa Ukawa
imeundwa kwa lengo la kuuvunja Muungano uliodumu kwa miaka 50 na
kudumisha amani na umoja kwa Tanzania.
Kinana akihutubia katika mkutano huo na kutamka kuwa CCMitasimia kidete kuhakikiasha uchumi wa Zanzibar unaimarika.
Kinana na viongozi wengine wakiuombea dua muungano wa Tanzania pamoja
viongozi waanzilishi wa muungano huo ambao ni Julius Nyerere na Abeid
Karume
Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akikemea kitendo cha viongozi wa
UKAWA kungea uongo na tabia ya kuwakejeli waasisi wa Muungano wa
Tanzania.
Mjumbe wa Bunge la Katiba,Asha Bakari Makame akimchana chana Katibu
Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad kwa tabia yake ya kinyonga kuhusu muundo
wa Muungano.
Mamboo poa/
Mjumbe wa Bunge la Katiba, Ummy Mwalimu akielezea jambo kuhusu mwenendo usi faa wa UKAWA kukimbia vikao vya bunge hilo
Mjumbe wa Bunge la Katiba Emmanuel Nchimbi akinukuuu kwenye kitabu
kilichotungwa na Maalim Seif Sharif Hamad kinachopinga Muungano
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo
ambapo alipingana na viongozo wanaowabebembeleza wananchama wa Ukawa
kurudi katika Bunge la Katiba, akidai waachwe kwani tangu walipoondoka
bunge limekuwa la kistaraabu/
No comments:
Post a Comment