madaktari walalamikia kutokamilika kwa miradi ya ujenzi vituo vya afya kwa wakati,wakulima wa tumbaku waangusha kilio chao cha kutolipwa fedha zao mbele ya Kinana wilayani sikonge
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya ujenzi wa jengo
la upasuaji na Dk.Sylvanus Kabutura Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya
cha Kata ya Kitunda wilayani Sikonge,Daktari Kabutura alimueleza Katibu
Mkuu wa CCM changamoto kubwa uhaba wa maji katika kituo hicho,na pia
kutokamilika kwa jengo kubwa la huduma za upasuaji na huduma nyingine
zaidi ya mwaka,jambo ambalo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
hakufurahishwa nalo,kwani kumekuwepo na malalamiko makubwa kutoka kwa
wananchi wilayani humo kwa ukosefu wa huduma mbalimbali za afya kwa
Wananchi kufuatia kutokamilika kwa jengo hilo na miradi mingine
mbalimbali ya zahanati iliyosababishwa na Mkandarasi aliyepewa tenda ya
ujenzi wa miradi hiyo,kwa wakati.
Mbunge wa Jimbo la Sikonge Said Mkumba akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (shoto),kati Dk.Sylvanus
Kabutura Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Kata ya Kitunda wilayani
Sikonge,pamoja na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnaye
wakimsikiliza.
Akitolea
Ufafanuzi zaidi kuhusua suala hilo,Mbunge wa Jimbo la Sikonge,Mh Said
Mkumba ameeleza kuwa,Mkandarasi wa ujenzi wa vituo hivyo vya
Afya,ameshindwa kumaliza kazi kwa wakati,wakati mkataba ulianza mnamo
28/10/2009 na ulipaswa kumalizika 2/5/2011,lakini mpaka sasa vituo hivyo
na zahanati havijakamilika,jambo ambalo limekuwa likikwamisha maendeleo
katika suala zima la Afya wilayani humo.
Mh.Mkumba
alizidi kubainisha kuwa kupitia Mradi wa Kupunguza vifo kwa akina mama
Support to Martenal Mortality Project Reduction (SMMRP).Jumla ya vituo
saba vya kutolea huduma za Afya Wilayani Sikonge vilitakiwa
kujengwa,vikiwa ni Kipili,Kitumbi,Tumbili,Pangale,Kitunda,Mazinge na
Kisanga,ambapo jumla ya shilingi bilioni 2,051,723,850 zimelipwa kwa
mkadarasi huyo,lakin hata hivyo kazi hiyo haijakamilika mpaka sasa.
Wananchi wa kijiji cha Lukula,katata ya Kitunda wakimsikiliza Mbunge
wa Jimbo la Sikonge Said Mkumba,wakati akielezea mambo mbalimbali
waliyoyatekeleza kupitia chama chake cha CCM,na pia akionesha ni namna
gani amekuwa akikerwa na kunyonywa kwa Wakulima wa zao la
Tumbaku,wilayani humo kupitia Vyama vya Ushirika,ambavyo vimefuja kiasi
kikubwa cha fedha na kuwaacha wakulima hao katika sintofahamu huku
maisha yao yakiendelea kuwa duni siku hadi siku.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha
Mgambo kitongoji cha Lukula kata ya Kitunda wilayani Sikonge mkani
Tabora ambapo aliwaomba radhi wakulima wa Tumbaku kwa kadhia waliyo nayo
kutokana na kunyonywa na kutopata haki zao za malipo kwa miaka 3.Kinana
aliongeza kuwa pamoja na kuwaomba radhi wakulima hao wa Tumbaku,amesema
waruhusiwa kuuza tumbaku yao wanapotaka,kwa sababu vyama vya ushirika
vya msingi vimekuwa vikiwadhulumu kwa kiasi kikubwa wakulima hao.Aidha
Kinana ameahidi suala hilo la dhuluma kwa Wakulima wa tumbaku na sualal
la Zahanati kuyafikisha kwa Dkt.Rais Jakaya Kikwete.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Mbunge wa Jimbo la
Sikonge Said Mkumba wakiwasomea wananchi wa kijiji cha Lukula maeneo
yatakayopata umeme mwaka huu katika wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.
Mkulima
wa zao la Tumbaku Lameck Mnyama akitoa ushuhuda na malalamiko ya
wakulima wa zao hilo,kwa namna ambavyo vyama vya ushiriki vimekuwa
vikiwaibia na kushindwa kuwalipa fedha zao kwa wakati
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikazia jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh.Fatma Mwasa na Katibu
wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnaye wakimsikiliza mara baada ya
kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Lukula katika
kata ya Kitunda,wilayani Sikonge.








No comments:
Post a Comment