Header Ads

KINANA ALAKIWA NA SAMUEL SITTA PAMOJA NA VIONGOZI WA CUF URAMBO


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua shamba la mahindi la Kikundi cha Vijana cha Hiari ya Moyo katika Kijiji cha Ndorobo, wakati wa ziara yake, wilayani Urambo, mkoani Tabora jana. Mahindi hayo yanazalishwa kwa kilimo cha umwagiliaji
 Kinanaakitoka kukagua kisima kichotumiwa na vijana wa Hiari ya Moyo kumwagilia mashamba yao
 Kinana akikagua gwaride la chipukizi wa CCM baada ya kuwasili wilayani Urambo.
 Kinana akikumbatiana na Diwani wa Kata ya Usoke, Kandora Nyanda (CUF), ambaye alikuwepo wakati wa mapokezi wilayani Urambo, Tabora ambako ameanza ziara ya kikazi ya  kuimarisha chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuata Ilani ya CCM mkoani, Tabora
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia wakati wa mapokezi ya msafara wa Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana katika Kijiji cha Izimbili, wilayani Urambo
 Kinana akijadiliana jambo na Mbunge wa Urambo, Samuel Sitta wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Izimbili, wilayani Urambo. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Fatma Mwassa, ambako ameanza ziara ya kikazi ya  kuimarisha chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuata Ilani ya CCM mkoani, Tabora
 Samuel Sitta akicheza ngoma iliyokuwa ikitumbiza wakati wa uzinduzi wa Zahanati ya Izengabotogilwe
 Vijana wa Sungusungu wakishangilia wakati wa uzinduzi wa Zahanati ya Izengabotogilwe yenye uwezo wa kuhudumia vijiji vinne, wakati zaiara yake wilayani Urambo
 Wananchi wakigombea kumsalimia Kinana baada ya kuzindua zahanati hiyo
 Kinana akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa kikundi cha Vijana cha wakulima wa mashamba ya umwagiliaji cha Hiari ya Moyo Kijiji cha Ndorobo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Jimbo la Urambo, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (kushoto), wakisaidia ujenzi wa jengo la CCM Tawi la Mabatini mjini Urambo,wakati wa ziara yake ya kuimarisha chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuata Ilani ya CCM mkoani, Tabora
 Sitta akiagua shamba la mahindi la kikundi cha vijana cha Hiari ya Moyo
 Vijana wa Chipuklizi wa CCM wakimlaki Kinana katika Kijiji cha Izimbili
 Wananchi wakishangilia wakati wa mapokezi ya Kinana katika Kijiji cha Izimbili
 Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Tabora, Magreth Sitta akiwasalimia wananchi wakati wa mapokezi ya Kinana katika Kijiji cha Izimbili, wilayani Urambo.
 Kinana akihutubia wananchi wakati wa mapokezi ya msafara wake katika Kijiji cha Izimbili
 Sungusungu wakishangilia baada ya Kinana kuzindua Zahanati Izengabotogilwe
 Kinana akiagana na Sungungusungu hao
 Kinana akizindua mradi wa wanawake wa mashine za kukamua alizeti katika Kijiji cha Itundu
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua wodi ya Mama Ngojea katika Hospitali ya Wilaya ya Urambo, mjini Urambo,. Jengo hilo limejengwa kwa msaada wa Mbunge wa Jimbo hilo,  Samuel Sitta, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Magreth Sitta, Mfanyabiashara maarufu Mustafa Sabodo na Halmashauri ya wilaya hiyo. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

No comments:

Powered by Blogger.