WATUMISHI OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA WAPIGWA MSASA JUU YA ELIMU YA UKIMWI MAHALA PA KAZI
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akifungua mafunzo ya Ukimwi
mahali pa kazi kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mwishoni
mwa juma, Semina hiyo iliyoandaliwa na idara ya maendeleo ya jamii na
mratibu wa TACAIDS Mkoa wa Rukwa kwa watumishi hao ilikua na lengo la
kuelimishana na kukumbushana juu ya mambo mbalimbali yanayohusu janga la
Ukimwi na umuhimu wa Tohara kwa wanaume katika kujikinga na janga hilo.
Katika hotuba yake Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa hakusita kuonyesha hisia
zake kali kwa watumishi watakaohusika katika rushwa za ngono na kusema
kuwa watachukuliwa hatua kali bila ya utetezi wowote kutoka kwake.
Mratibu
wa TACAIDS Mkoa wa Rukwa Ndugu Daniel Mwaiteleke akitoa mada juu ya
uelewa wa jumla kuhusu gonjwa la UKIMWI kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa Rukwa katika mafunzo ya siku moja yaliyofanyika katika ukumbi wa
RDC Mjini Sumbawanga.
Muwezeshaji
wa mada ya magonjwa ya zinaa STD na STI Dkt. Lunyelele akiwasilisha
mada yake kwa umahiri mkubwa bila ya kutafunatafuna maneno.
Dkt. Lunyelele akiwa anatoa mafunzo hayo.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mafunzo hayo.
Mjumbe katika Semina hiyo Ndugu Frank Mateny akichangia moja ya mada katika mafunzo hayo.
Mdau Mussa Mwangoka na Paul Ngany'anyuka ndani ya Semina hiyo.
Dena na Richard Ndambala nao walikuwepo.
(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment