TAARIFA NA LUGHA SAHIHI: DHANA YA KUPUNGUZA MADHARA YA MAAFA
Meneja
wa kituo cha Kahama FM Redio, Marco Mipawa, akiwakaribisha washiriki na
kufungua warsha ya mafunzo ya siku nne ya waandishi wa habari na
watangazaji wa Redio Jamii kuhusu kuandika taarifa za Maafa na Misaada
ya Kibinadamu yanayofanyika mjini Kahama. Kushoto ni Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu na kulia ni Hellen Msemo kutoka Mamamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA).
Na Mwandishi Wetu.
Ukosefu
wa taarifa na lugha sahihi halikadhalika kukosa uelewa katika jamii ni
miongoni mwa mambo yanayosababisha kutokea kwa maafa. Katika
mada inayohusu Misaada ya Kibinadamu na Taarifa za Maafa katika mafunzo
ya siku nne ya wanahabari na watangazaji wa redio jamii mjini Kahama
Mratibu wa idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bwana Harrison
Christopher Chinyuka alisema jamii lazima ifahamu historia ya maeneo
yanapotokea maafa na wapate elimu ya kutosha ili waweze kuepusha maafa
asili.
Bwana
Chinyuka alisema kwamba hilo litafanikiwa iwapo waandishi wa habari
watawajibika kikamilifu kwa kuandika taarifa za majanga na maafa ambazo
ni sahihi na kwa wakati kwa sababu wakati mwingine wamekuwa wakishindwa
kutumia lugha sahihi ya kusheheneza taarifa husika.
Mratibu
wa Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bwana Harrison
Christopher Chinyuka Chinyuka, akiendesha mafunzo kwa waandishi na
watangazaji wa Redio za Jamii nchini.
“Wanahabari wana mchango mkubwa katika kuhakikisha kuwa madhara ya
maafa yanapunguzwa kwa kuipa uelewa jamii husika kwa kutoa taarifa na
lugha sahihi zinazohusu maafa ili kutoa nafasi kwa wahanga kujihami
ipasavyo”, alisema Bwana Chinyuka.
Wajibu
wa mwandishi wa habari katika kupunguza maafa ni kukuza uelewa wa jamii
kuhusu hatua za hatari, kuzuia na kukabiliana na maafa, kukubaliana juu
ya viwango vya taratibu za uendeshaji katika sehemu ya maafa.
Wajibu
mwingine ni kusambaza ujumbe wa onyo kwa kuaminika na haraka
iwezekanavyo na kuiweka jamii vizuri kitaarifa wakati huo huo kuepuka
uvumi na hofu katika hali ya hadhari.
Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu, akihamaisha washiriki katika vikundi kazi.
No comments:
Post a Comment