PICHA : MPIGA GITA WA SKYLIGHT BAND CHIRI CHALLA AZIKWA JIJINI DAR ES SALAAM
MPIGA
gitaa wa bendi ya Skylight, aliyefariki juzi katika Hospitali ya
Muhimbili jijini Dar es Salaam, Chiri Challa, amezikwa katika makaburi
ya Mwananyamala kwa Kopa, Kinondoni jana na kuhudhuriwa na wadau
mbalimbali.
Awali uongozi wa bendi hiyo
kupitia kwa Meneja wake, Aneth Kushaba ‘AK47’, ulieleza kuwa mwanamuziki
huyo alifariki kutokana na ugonjwa wa kupooza nusu ya mwili wake, hali
iliyosababisha kutofanya kazi ipasavyo.
Kushaba alibainisha kuwa kupooza
huko kulisababisha mishipa ya damu kichwani kupasuka na kumsababishia
maumivu makali sehemu za kichwani.
“Tunatoa pole kwa familia ya
marehemu na mashabiki wetu wote katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa
mpendwa wetu,” alisema Kushaba.
No comments:
Post a Comment