PICHA KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS-IKULU:MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA MRADI WA MAISHA, UNAOHUSU AFYA YA MAMA NA MTOTO, JIJINI DAR ES SALAAM
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiangalia na kupata maelezo kutoka kwa Meja Ali Kitundu, kuhusu elimu ya awali
kwa wanafunzi wanaojifunza elimu ya afya kabla ya ajila., wakati alipofika
kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kufungua Kongamano
la Mradi wa Maisha kuhusu Afya ya Mama na Mtoto. Kutoka kulia ni Dkt. Grace Qoro, Waratibu wa
mradi huo, Jasmine Chechewa na Shallah Ukende.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza
maelezo jinsi ya kumhudumia mama mjamzito kutoka kwa Mratibu Msaidizi wa Afya
Mzazi na Mtoto wa Wilaya ya Ilala, Edith Mboga, wakati alipofika kwenye Hoteli
ya Serena jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kufungua Kongamano la Mradi wa
Maisha kuhusu Afya ya Mama na Mtoto. Kulia
ni Mshauri wa Ukunga Mradi wa Maisha, Scholastica Chibehe.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia,
wakati alipofika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya
kufungua Kongamano la Mradi wa Maisha kuhusu Afya ya Mama na Mtoto.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi
cheti mwakilishi wa Mradi wa Maisha kutoka Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa
Mmbando, wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano la Mradi wa Maisha kuhusu Afya
ya Mama na Mtoto, jijini Dar es Salaam, leo.
No comments:
Post a Comment