Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba, Azuia Benki kuwalipa "UKAWA" waliokimbia Bungeni
![]() |
| Naibu waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba |
Naibu
Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Lameck Nchemba, Ikiwa ni Siku ya pili tangu
Wajumbe wa Bunge la Katiba Kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo,Cuf
na NCCR Mageuzi wanaounda kitu kinachoitwa UKAWA wasusie Shughuli za
Bunge la Katiba kwa Madai wamechoka Kutukana na Kuburuzwa kwenye Bunge
hilo.
Hii
leo Naibu waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba ambaye kwa Sasa anakaimu
Kuwa Waziri wa Fedha tangu Tarehe.10./04/2014 hadi 18/04/2014 kutokana
na Waziri wa Fedha kusafiri Nchini Marekani Kikazi,amefuta Malipo ya
wabunge waliosusia Mchakato wa Katiba.
Habari
za Uhakika Kutoka Chanzo chetu ndani ya hazina kinasema,Mwigulu Nchemba
ameagiza Mabenki yote kurudisha Cheque za Malipo ya Posho na seating
allowance zilizopelekwa na Bunge jana tar.16/04/2014 ili ziwekwe kwenye
akaunti binafsi za Wabunge ikiwa ni Malipo ya Mpaka tar.30/04/2014.Pia
ilikujiridhisha na taarifa hizo,Mwandishi wetu alizungumza na Wajumbe
namna Mtiririko wa Malipo unavyofanyika ndani ya Bunge hilo,Mjumbe(Jina
tunalihifadhi) alisema fedha zote zinapitia Benki na wakati
wanajiandikisha siku za Kwanza walitakiwa Kuandika namba zao za Benki na
Malipo yote hupitia huko,hivyo kama ni fedha zinazuiliwa Benki.
Baadhi
ya wabunge wa CUF na Chadema wanaojiita UKAWA toka jana walijua
wameshasaini fedha hizo hivyo zitaingia kwenye account zao Binafsi.
Mambo yamekuwa tofauti baada ya Naibu Waziri wa Fedha(Sera) Mh:Mwigulu
kuagiza leo form zisainiwe upya leo na zitasainiwa pia tar 22 mpaka
25,Kwa madai ya asiyefanya kazi na asile.
Mbali
na hilo,Mh:Mwigulu amenukuliwa na clouds fm akisisitiza Rais kuwafuta
wajumbe wakiojitoa na badala yake awateue watu waliotayari kutunga
katiba hata bure kuliko hawa wanaokutana vikao lukuki kupanga njama za
kususia mchakato. Aidha Mwigulu alisema fedha inayotumika ingeweza
kulipwa Wazabuni wanaozidai halmshauri, wangeweza kulipa madeni ya
walimu, au kuwapa mikopo watoto wa masikini waliofaulu ila hawajaenda
vyuo kwa kukosa mikopo, au zingenunua madawa hosipitalini, au
zingepeleka umeme, maji, vitabu au barabara lakini wamelipwa wajumbe
badala ya kufanya kazi hiyo wanapanga njama ya kuhujumu mchakato
usiendelee kwa kutafuta visingizio lukuki.
Bunge
la Katiba linategemewa kuendelea Tar.22 Mwezi huu mara baada ya sikukuu
za Pasaka Kupita na litaahirishwa tena Tar 25 mwezi huu kupisha Bunge la
Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:
Post a Comment