KINANA ATINGA JIMBO LA WAZIRI MKUU PINDA, AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipongezwa na wazee wa Kijiji
ya Majimoto, wilayani Mulele, mkoani Katavi baada ya kusimikwa kuwa
mmoja wa wazee wa kabila la wasukuma wakati wa mkutano wa hadhara katika
kijiji hicho, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua
miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM.PICHA ZOTE
NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Kinana akihutubia umati wa wananchi katika kijiji cha Majimoto.
Kinana akiwa na viongozi wengine wa chama na serikali wakiangalia
shamba la ufuta la Waziri Mkuu Mixengo Pinda katika Kijiji cha Kibaoni,
Wilaya mpya ya Mulele, mkoani Katavi wakati wa ziara yake.Pia alikagua
mradi wa nyuki katika shamba hilo.
Mkazi wa Kijiji cha Usevya, Wilaya ya Mulele, Benard Juta akishangilia
wakati Katibu Mkuu wa CCM, Kinana alipowasili katika kijiji hicho.
Vijana wakionesha ramani ya wilaya mpya ya Mulele, ambayo Mkuu wa Wilya
ya hiyo alidai ni kubwa na kuomba serikali igawanye kupata wilaya
ingine ya Nsimbo.
Katibu Mkuu wa CCM,Kinana 9kushoto), Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape
Nnauye ( wa pili kulia) na Mjumbe wa Nec, Balozi Ali Abeid Karume
(kulia), wakiwa nyumbani kwa wazazi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Wa
pili ni mamake Pinda na mdogo wake.
Kinana akiwa na mamake Pinda katika Kijiji cha Kibaoni, wilayani Mulele.
Nape akiwa amembeba mjukuu wa Pinda aitwaye Pinda.
Kinana akiagana na mamake Pinda. Kulia ni Karume na kushoto ni Nape wakisubiri kuagana naye
Kinana akikagua ujenzi wa mradi wa maji katika Kijiji cha Kibaoni
wilayani Mulele, Katavi. Mbunge wa Jimbo la Katavi ni Waziri Mkuu Pinda.
Kinana akiwa katika shamba la ufuta lia Waziri Mkuu, Pinda lililopo katika Kijiji alichaozaliwa waziri mkuu huyo
Kinana akikagua mradi wa mashine za kuchambua na kukoboa mpunga katika
Kijiji cha Mwamapuli, wakati wa ziara yake wilayani Mulele
Kinana akisaidiana na wananchi kusomba matofali ya kujengea Shule ya Msingi Majimoto, wakati wa ziara yake wilyanai Mulelke.
Nape akisaidiana na wananchi kusomba matofali ya kujengea shule hiyo.
Kinana akiwa amebeba ndoo yenye zege la kujengea msingi wa shule hiyo
Nape akijumuika kucheza ngoma ya zeze ya kabila la wasukuma wakati wa
mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Majimoto, wilayani Mulele, Mkoa wa
Katavi.
Mjumbe wa NEC-CCM,Balozi Ali Abeid Karume akihutubia katika mkutano wa
hadhara katika Kijiji cha Majimoto, na kuwataka wananchi kuunga mkono
muungano wa serikali mbili katika mchakato wa kuunda Katiba Mpya.
Nape akiunguruma katika mkutano huo wa hadhara ambapo alilaani kitendo
cha CHADEMA kumtuma Tundu Lissu kumtukana Baba wa Taifa Julius Nyerere
katika vikao vya Bunge Maalum la Katiba linaloondelea Dodoma.
Kinana akiwa amevishwa mgolole na kupewa silaha za jadi aliposimikwa na
wazee wa Kisukuma kuwa mmoja wa wazee wa kabila hilo wakati wa mkutano
wa hadhara katika Kijiji cha Majimoto, wilayani Mulele.
Sehemu ya umati wa wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara
uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana katika Kijiji cha Majimoto,
Wilaya mpya ya Mulele, mkoani Katavi. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD
MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
No comments:
Post a Comment