Katibu wa CHADEMA Jimbo la Mufindi Kusini, Emannuel Ngwalanje , Ahamia CCM
Emmanuel Ngwalanje akitoa yake yaliyokuwa moyoni kwa wananchi kabla ya kujiunga na CCM.
Katibu
wa Chadema Jimbo la Mufindi Kusini, Emannuel Ngwalanje akikabidhi
vitendea kazi vyake na kadi ya Uanachama wa CHADEMA kwa katibu wa CCM
wilaya ya Mufindi Miraji Mtaturu (kushoto ) baada ya kukihama chama
hicho na kujiunga na CCM
Aliyekuwa
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Mufindi Kusini, Emannuel Ngwalanje akipewa
vitendea kazi vya CCM na kadi ya Uanachama baada ya kujiunga na chama
chenye umoja na mshikamano, CCM.
======= ===== =======
MZIMU
wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Zitto Kabwe umeelezwa kumkimbiza hadi Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Katibu wa Chadema jimbo la Mufindi Kusini, Emannuel Ngwalanje.
Hatua
ya Ngwalanje kujitoa Chadema na kujiunga na CCM imeelezwa na baadhi ya
wafuasi wa Chadema kuwa ni pigo kubwa kwa chama hicho.
Akizungumzia
kujitoa kwa Ngwalanje, mwanachama wa Chadema Michael Ngimbusi alisema;
“Ngwalanje alikuwa nguzo kuu ya Chadema wilayani Mufindi, aliogopwa na
wana CCM, hiyo ikiwa ni kutokana na uwezo wake mkubwa wa kushawishi na
kujenga hoja.
Katika
kipindi cha zaidi ya miaka minne ambacho Ngwalanje amekuwa Katibu wa
Chadema jimbo la Mufindi Kusini ameweza kushawishi zaidi ya wakazi 600
katika maeneo mbalimbali jimboni humo kujiunga na chama hicho.
Katika
mkutano wa mapokezi yake uliofanyika kijijini kwake Kimilinzowo kata ya
Itandula alisema; “Kazi ya kuibomoa Chadema haitaishia katika wilaya ya
Mufindi pekee, bali nitaiendeleza hadi Jimbo la Iringa Mjini
linaloongozwa na Mchungaji Peter Msigwa kupitia Chadema.” Ngwalanje
alisema utawala mbovu na matumizi mabaya ya fedha za ruzuku
utaisambaratisha Chadema katika kipindi kifupi kijacho.
Alisema
chama hicho kinapata fedha nyingi zinazotokana na ruzuku ya serikali na
michango ya wanachama, wafuasi na marafiki zake wa ndani na nje ya nchi
lakini zimekuwa zikiwanufaisha wachache.
Alisema
wakati kundi kubwa la viongozi wa chama hicho likifanya kazi kwa
kujitolea, kundi la wachache walioko makao makuu wamekuwa wakitafuna
fedha hizo bila woga huku wakiwatishia wanaohoji.
Alisema demokrasia
inayohubiriwa kutafutwa na chama hicho nchini ina walakini kwa
kuzingatia kwamba ndani ya chama hicho zipo nafasi za uongozi ambazo kwa
wengine ni uhaini kuziwania.
Kwa hisani ya Habarileo.
No comments:
Post a Comment