KATIBU MKUU WA CCM,KINANA AZINDUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA 60 ZA NHC WILAYANI MLELE LEO
Katibu
Mkuu wa CC,Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe na kuweka jiwe la
msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba 60 za Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC),katika kijiji cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo jioni.
Meneja wa Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC),mkoa wa Katavi,Bwa.Nehemia Msigwa akifafanua
zaidi kuhusiana na mradi huo kwa katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mara
baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa
nyumba 60 za Shirika hilo,katika kijiji cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya
ya Mlele mkoani Katavi leo.
Meneja
Huduma kwa jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),makao Makuu jijini
Dar,Bwa.Muungano Sagaya akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
na Ujumbe wake kwenye uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa nyumba 60 za
Shirika hilo,katika kijiji cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya ya Mlele
mkoani Katavi mapema leo jioni.
Meneja wa Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC),mkoa wa Katavi,Bwa.Nehemia Msigwa akizungumza
mbele ya mgeni rasmi,katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kabla ya kuweka jiwe
la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba 60 za Shirika hilo,katika kijiji
cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo
jioni.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mh.Rajab Rutengwe akizungumza jambo kabla ya katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuweka jiwe
la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba 60 za Shirika hilo,katika kijiji
cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo
jioni.
Meneja wa Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC),mkoa wa Katavi,Bwa.Nehemia Msigwa akizungumza
jambo na Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mh.Rajab Rutengwe kabla ya katibu Mkuu
wa CCM,Ndugu Kinana kuweka jiwe la msingi la mradi wa
ujenzi wa nyumba 60 za Shirika hilo,katika kijiji cha Inyonga ndani ya
Wilaya Mpya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo jioni.
Katibu Mkuu wa CC,Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),mkoa wa Katavi,Bwa.Nehemia Msigwa kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba 60 za Shirika hilo,katika kijiji cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo jioni.
======== ====== =====
KATIBU Mkuu wa CCM amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC), kwa kasi ya ujenzi miradi ya nyumba za makazi na biashara kwenye miji
mbalimbali hasa makao makuu ya wilaya mpya.
Kinana aliyasema hayo katika mji wa Inyonga wilayani Mlele
mkoa wa Katavi wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba 60 za shirika
hilo.
Alisema uongozi mpya wa NHC umerudisha heshima na hadhi ya
shirika hilo kwa kufanya kazi ambazo inapaswa kuzitekeleza.Kwa mujibu wa Kinana, katika kipindi cha karibuni NHC,
imekuwa ikitekeleza kwa kazi miradi ya ujenzi wa nyumba za viwango mbalimbali
ambazo ni muhimu na kimbilio la watu wa kipato cha chini.
"Hii ndio kazi inayopaswa kufanywa na shirika la nyumba
ambalo ni tegemeo la wananchi. CCM inatambua kazi mnayoifanya inakupongezeni na
kuungeni mkono katika kutekeleza majukumu yenu," alisema.
Akizungumza kuhusu kilio cha kutaka kupunguziwa kodi kwenye
vifaa vya ujenzi vya shirika hilo, Kinana alisema hoja hiyo ni muhimu na
inayopaswa kusikilizwa na kupewa kipaumbele kwa lengo la kuwasaidia watu wa
kipato cha chini.
"Naona hapa kuna hoja ya msingi kwa kuwa hakuna sababu
ya kutoza kiwango kibwa cha kodi kama nyumba zinazojengwa zinawasaidia watu wa
kipato cha chini wakiwemo watumishi wa umma wenye mishahara midogo,"
alisema.
Kwa upande wake, Meneja wa NHC mkoa wa Katavi, Nehemia
Msigwa, alisema nyumba hizo 60 zitajengwa kwa kipindi cha miezi minane.
Alisema zitakapokamilika, nyumba hizo zitauzwa kwa bei
tofauti huku ya juu ikiwa ni sh milioni 54 na ya chini sh milioni 38.
Msigwa alisema nyumba hizo ni sehemu ya utekelezaji wa
mkakati wa NHC kujenga nyumba 15,000 kwa kipindi hadi mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment