KATIBU MKUU WA CCM,KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI KATAVI
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa
Afisa Zana za Kilimo wa Wilaya ya Mlele,kuhusiana na Mradi wa Mashine ya
Kusindika Mpunga mapema leo jioni,katika kijiji cha Mwampuli,Wilaya
mpya ya Mlele mkoani Katavi,Mashine hiyo ina uwezo wa kusindika mpunga
tani 30 kwa siku.Kushoto ni Mjumbe wa NEC Taifa,Balozi Ali Karume nae
akisikiliza kwa makini.Kinana yupo Mkoani Katavi kwa ziara ya siku nne
ya
kuimarisha uhai wa chama,kukagua na kuhimiza ilani ya Uchaguzi ya 2010.
Mradi
wa Mashine ya Kusindika Mpunga kama uonekavyo pichani uliopo katika
kijiji cha Mwampuli,Wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi,Mashine hiyo ina
uwezo wa
kusindika mpunga tani 30 kwa siku.
Katibu
Mkuu wa CCM,akikagua Ujenzi wa Mradi wa Maji safi,katika kijiji cha
Kibaoni,Wilaya ya Mlele,mkoani Katavi.Tanki hilo la maji safi
linatarajia kuhudumia wakazi wa kijiji cha Kibaoni na vijiji vingine
tisa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wa tatu kulia akishiriki kukusanya mawe pamoja na viongozi mbalimbali wa Taifa,Mkoa na Wilaya (CCM),kukusanya mawe kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa shule ya msingi Maji Moto iliyopo katika kijiji cha Maji Moto,Wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi. Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Maji Moto jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara,Nape amewataka wana CCM na wananchi kwa ujumla kuishi kwa amani na upendo katika suala zima la kudumisha amani tulionayo na kuwapuuza wanaotaka kuleta mgawanyiko katika nchi yetu kwa namna moja ama nyingine.

Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Maji Moto
jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara,Kinana ameeleza kuwa kumekuwepo
tatizo kubwa kila mahali aendapo kufanya ziara kuhusiana na migogoro ya
ardhi kati ya Wakulima na Wafugaji,Wafugaji na Hifadhi,jambo ambalo
linapaswa kufanyiwa kazi kwa umakini mkubwa sana,aliongeza kuwa migogoro
hiyo imekuwa janga la Taifa,kutokana na idadi ya watu kuongezeka katika
maeneo mengi,huku mipaka yake kubaki kama iliyo kwa muda mrefu.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mama Mzazi wa
Waziri Mkuu,Mh Pinda, mapema mchana huu nyumbani kwake,Katika kijiji cha
Kibaoni Wilaya Mlela mkoani Katavi,alipokwenda kumtembelea na kumjulia
hali.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Mama Mzazi wa
Waziri Mkuu,Mh Pinda, mapema mchana huu nyumbani kwake,Katika kijiji
cha Kibaoni Wilaya Mlele mkoani Katavi,alipokwenda kumtembelea na
kumjulia hali.Kinana yuko Mkoani Katavi kwa ziara ya siku nne ya
kuimarisha uhai wa chama,kukagua na kuhimiza ilani ya Uchaguzi ya 2010.
Kinana
akijaribu kuelewesha jambo katika shamba la Ufugaji nyuki la Waziri
Mkuu Pinda,katika kijiji cha Kibaoni Wilaya ya Mlele mkoani Katavi
mapema leo mchana.
Kinana akikatiza kwenye Shamba la Ufuta na Nyuki mara baada ya kujionea ufugaji wa nyuki unavyofanyika.
No comments:
Post a Comment