JAMII IMETAKIWA KUTUMIA VYAKULA VINAVYOPATIKANA KATIKA MAZINGIRA YANAYOWAZUNGUKA KUBORESHA AFYA ZA FAMILA ZAO
Afisa
kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Valerian Vitalis
Kidole, akiendesha mafunzo ya siku nne ya wanahabari na watangazaji wa
redio jamii yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa
kushirikiana na UNESCO yaliyofanyika katika ukumbi wa Kartasi uliopo
wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Na Mwandishi wetu.
Wito
huo umetolewa na Afisa kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika,
Bw. Valerian Vitalis Kidole katika semina ya siku nne kwa waandishi wa
habari na watangazaji wa redio jamii iliyomalizika mwishoni mwa katika
ukumbi wa Kartasi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Kidole
alisema kuwa ili kuhakikisha jamii inapata lishe haina budi kutumia
vyakula vile vinavyopatikana katika maeneo wanamoishi kuliko kusubiri
vyakula vya msaada kutoka serikalini na vyakula kutoka viwandani.
Hayo
yamezungumzwa katika mafunzo ya Kupunguza Madhara ya Maafa na kutoa
Msaada wa Dharura yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden
(SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO kwa ajili ya waandishi wa Habari na
watangazaji wa redio jamii yanayofanyika Kahama wakati mwezeshaji akitoa
mada ya Usalama wa Chakula nchini.
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa chakula hutoa msaada
wa chakula kwa wananchi pale kunapotokea upungufu wa chakula katika
maeneo husika.
Aidha Kidole amesema kuwa chakula cha msaada kinachotolewa na serikali ni nafaka ambayo hayawezi kuboresha afya zao. Katika
halmashauri za mikoa nchini ambazo zina upungufu wa chakula, viongozi
wa ngazi husika hawana budi kuwaelimisha wanachi juu ya kulima mazao
mengi yanayohimili hali ya hewa husika na kwa wakati mwafaka ili
kupunguza tatizo la upungufu wa chakula katika maeneo yao. Ni kwa namna
hiyo jamii itaipunguzia serikali mzigo wa kutoa chakula cha msaada na
badala yake kufanya shuguli nyingine za maendeleo.
No comments:
Post a Comment