Baraza Kuu la Wafanyakazi NSSF Lakutana Dar es Salaam
picha
ya pamoja baada ya mkutano wao wa siku mbili uliofanyika jijini Dar es
Salaam.[/caption]
BARAZA Kuu la Wafanyakazi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
limekutana kwa siku mbili jijini Dar es Salaam tangu juzi kufanya vikao
vyake vya kazi ikiwa ni pamoja na kuangalia utendaji kazi, kupitia
mikakati na malengo mbalimbali iliyojiwekea.
Mkutano
huo ambao pia umejadili na kupitisha bajeti ya shirika kwa mwaka
2014/15 umeongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, ambaye pia ni
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani K. Dau na kufanyika katika Ukumbi
wa Mikutano wa NSSF uliopo Katika Jengo la shirika hilo 'WeterFront
House' la jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo umejumuisha Watendaji Wakuu toka Makao Makuu, Mameneja wa
Mikoa, Watendaji wa kuu wa mikoa na wajumbe wengine wanaounda baraza la
wafanyakazi la NSSF.
Jumla
ya wajumbe 142 wameshiriki katika mkutano huo uliofanyika kwa siku
mbili. Shirika la NSSF ni miongoni mwa mwashirika makubwa ya hifadhi ya
jamii nchini yenye vitega uchumi lukuki na vya thamani kubwa
vinaochangia kukua kwa uchumi wa taifa.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment