PICHA NA TAARIFA:TAMWA WATOA ELIMU KWA WABUNGE WANAWAKE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA KUZINGATIA MASUALA YA USAWA WA KIJINSIA WAKATI WA UTUNZI WA KATIBA MPYA

Mwenyekiti wa Wabunge wanawake Anna Abdallah (kulia) akifungua semina ya Wabunge wanawake wa Bunge Maalum la Katiba jana mjini Dodoma uliokuwa ukijadiliana juu ya umuhimu wa kuwekwa kwa umri wa mtoto katika Katiba mpya na umri unatakiwa kuolewa na kuoa na masuala ya uzazi salama. Kushoto ni NaibuWaziri wa Katiba na Sheria Mhe Angelah Kairuki.

Mjumbe wa Bunge la Katiba ambaye pia Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Dkt Pindi Chana akitoa maoni yake jana mjini Dodoma wakati wa semina ya Wabunge wanawake wa Bunge Maalum la Katiba uliondaliwa na Chama cha Waandishi wanawake Tanzania (TAMWA) juu ya kuwaelimisha masuala mbalimbali ya kuzingatia wakati wa utungaji wa Katiba mpya ikiwemo uzazi salama na kutoa ufafanuzijuu ya umri wa mtoto.
No comments:
Post a Comment