Mtoto wa Miaka 8 alivyojaribu kumuokoa baba yake kwenye ajali ya gari iliyochukua uhai wa Paul Walker
Mtoto
wa miaka 8 alijaribu kufanya kitendo cha kishujaa kumuokoa baba yake
‘Roger Rodas’ dereva mstaafu wa mashindano ya magari aliyepoteza maisha
kwenye ajali ya gari iliyochukua maisha ya star wa action movie ya ‘Fast
and Furious’ Paul Walker, ajali iliyotokea November 30.
Kwa
mujibu wa Radar Online, mtoto huyo wa Roger Rodas aliyekuwa dereva wa
gari hilo alikuwa mmoja kati ya watu wa kwanza kufika kwenye eneo la
tukio dakika kadhaa baada ya gari hilo kupata ajali na kushika moto.
Shuhuda
wa tukio hilo aliiambia Radar Online kuwa mtoto huyo aliruka uzio na
kwenda kwenye gari hilo lililokuwa likiendelea kuwaka moto kujaribu
kumuokoa baba yake lakini hakuweza kufanya chochote.
Roger Rodas alikuwa rafiki wa karibu wa Paul Walker na mshauri wake katika maswala ya biashara.
No comments:
Post a Comment