Dk Kitila Mkumbo Avuliwa Uongozi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Dk Kitila Mkumbo
---
Taarifa zilizotufikia, zimeeleza kuwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam umemvua madaraka kwa muda, Dk Kitila Mkumbo kuongoza Kitivo cha
Elimu cha Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam (DUCE).
LEO
imefahamika kwamba Dk Kitila amevuliwa madaraka hayo kwa muda
usiojulikana baada ya uongozi wa chuo hicho kupata taarifa kwenye vyombo
vya habari kuwa ni kiongozi wa Chadema huku akiwa mtumishi wa umma.
Baada ya uamuzi huo Dk Kitila ataendelea kuwa mhadhiri mwandamizi kwenye
kitivo hicho. Kwa mujibu wa uongozi wa chuo hicho, ni kinyume cha
sheria cha nchi mfanyakazi wa umma kuwa kiongozi katika chama cha siasa.
Kutokana na uamuzi wa chuo hicho wiki iliyopita Dk Kitila alipewa barua
ya kusimamishwa.Hivi karibuni Dk Kitila Mkumbo alivuliwa nafasi ya
Mjumbe wa Kamati Kuu
ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kushiriki
kuandika waraka wa badiliko ndani ya Chadema.
No comments:
Post a Comment