Header Ads

Mbunge wa Kigoma Kaskazini-Chadema ,Zitto Kabwe Aung'uruma Uwanja wa Mwanga Centre, Kigoma Mjini Nakusema :''Mimi nachukua kadi ya uanachama wa Chadema mwaka 1993 Wakati Huo,Katibu Mkuu wa Chadema Dk Wilbrod Slaa akiwa bado yuko CCM.


Mbunge wa Kigoma kaskazini, Zitto Kabwe akihutubia Wakazi wa Kijiji cha Bitale alipokuwa katika ziara ya kutembelea baadhi ya Vijiji.Picha na Anthony Kayanda  
---
 .Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe, amejibu mashambulizi kwa viongozi wa Chadema, kutokana na kile alichosema wanazunguka na kusema maneno yasiyo ya ukweli.

Akihutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika Uwanja wa Mwanga Centre, Kigoma mjini, alisema alichukua kadi ya uanachama wa Chadema mwaka 1993 wakati huo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa akiwa bado yuko CCM.
 
“Wakati hao wenye midomo mikubwa wanaoongea sasa, walipokuwa wamekumbatia watawala, nyinyi mlikuwa mnapigwa mabomu kutaka mageuzi, eti leo wao wapinzani zaidi kuliko sisi na ndiyo maana hatuwezi kuwaachia.
 
Hatuwezi kukubali, hatutoki, demokrasia ni mchakato na mwenzenu nimekuwa kwenye mchakato huu. Kadi yangu ya Chadema nimeichukulia kwenye uwanja huu, tarehe moja mwezi wa nne mwaka 1993, nikiwa na miaka 16, wakati nachukua kadi yangu, Katibu Mkuu wa chama changu alikuwa yuko CCM.
 
Akizungumza kile alichosema ni uongo unaosambazwa na viongozi wa juu wa chama hicho, Katibu Mkuu Dk Slaa na Mwenyekiti wake Mbowe waligawana maeneo Mbowe akaenda Kanda ya Ziwa na Dk Slaa Kanda ya Magharibi.Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea......

No comments:

Powered by Blogger.